Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 539
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hata leo, katikati ya misiba isiyohesabika na isiyoweza kuvumilika, Ummah huu umethibitika kuwa thabiti katika kitambulisho chake na hivyo hauwezi kuangamizwa. Imethibitika kuwa unastahiki vyeo ulivyotunukiwa na Mola wa walimwengu, Mwenyezi Mungu Azza wa Jall! Angalia Kashmir, India, Afghanistan... Angalia Waislamu wa Syria, Turkestan Mashariki, Myanmar, katika nchi za Afrika, duniani kote, na mwisho kabisa Waislamu wa Palestina na hasa Gaza! Magaidi hao wa Kizayuni wameshindwa katika kila lengo lao kuhusu Gaza. Ummah huu umethibitisha mara kwa mara, kwamba uwepo wake hauzimiki! Hata adui zake wawe wakatili kiasi gani!
Mfano wa Ukraine Unathibitisha Hatari ya Ukoloni wa Kijeshi!
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa amali kubwa za usiku katika idadi kadhaa ya miji Uturuki kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne tarehe 18/03/2025.
Moja ya sababu zilizomfanya msaliti Hasina kupinduliwa na watu ni kwamba alitekeleza njama ya India kule Pilkhana na mara kwa mara alifanya majaribio mabaya yote ya kuweka udhibiti wa India juu ya jeshi la nchi hiyo. Wakati ambapo wananchi wanapaza sauti kudai haki kwa mkasa wa Pilkhana, doria ya pamoja 'CORPAT' na zoezi la pande mbili 'Bangosagar' lililofanyika katika Ghuba ya Bengal kwa kushirikisha jeshi la wanamaji la Bangladesh na India imewashtua watu. Kwa kweli, vibaraka wa Marekani-India wamedhamiria kulinda maslahi ya kijiografia ya wakoloni wao hata kwa gharama ya ubwana wa nchi. Inafaa kutaja kwamba wakati matabaka ya kisiasa ya kisekula ya nchi hayakupaza sauti yake dhidi ya njama hiyo ya Pilkhana, ni Hizb ut Tahrir pekee ndiyo iliyofichua njama hiyo mbele ya taifa hilo kwa ushujaa na kupinga njama hiyo dhidi ya ubwana wa nchi hii.
Katika Uislamu, hakuna fahamu ya kuingia Jannat kulingana na nani unamjua na hadhi yako ya kidunia ni ipi. Wote walisifiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu ya sifa zao za pamoja za kuwa karibu katika utendaji wao wa kuwa kama mfano wa Mtume (saw). Ikiwa tunataka hadhi sawa ya kuingia Jannat lazima basi tufuate mfano wao wa kufanikiwa. Sifa zifuatazo basi zinahitajika.
Mafanikio yanazunguka ulimwengu huu na Akhera, anayemcha Mwenyezi Mungu (swt) humsahilishia mambo yake, hubariki matendo yake, huitengenezea nafsi yake, mke wake na watoto wake, humpa njia ya kutokea katika matatizo, humruzuku kutoka katika vyanzo asivyotarajia, na humtosheleza. Zaidi ya hayo, Yeye (swt) humlipa sana subira yake wakati wa matatizo. Wengine wamesema: "Mafanikio ni kupata ushindi na kufikia lengo la mtu. Katika dunia hii, maana yake ni kupata furaha inayoleta kutosheka katika maisha. Katika Akhera, ina jumuisha mambo manne: uwepo milele usio na mwisho, heshima bila fedheha, mali bila umasikini, na elimu bila ya ujinga."
Kwa wengi, “Falah” ina maana ya kupata sehemu kubwa zaidi ya starehe katika ulimwengu huu—kujilimbikizia mali nyingi, kushikilia vyeo vya juu, kuishi katika anasa na ubadhirifu, na kupata mafanikio mengi katika masomo, kazi, na maisha ya familia...
Ramadhan inapoingia katika maisha yetu kila mwaka, huleta mabadiliko-wakati wa uwazi ambapo tunarudi nyuma kutoka kwa mazoea yetu ya kila siku na kujiuliza maswali ya kina. Ni mwezi ambapo kwa kawaida tunatathmini upya uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu (swt), vipaumbele vyetu, na mwelekeo wa maisha yetu. Katika wakati huu mtakatifu, tunaanza kutafakari: Je, Mafanikio yanamaanisha nini hasa?
Kutokana na mauaji makubwa ya halaiki yanayotokea Gaza na dori ya Marekani katika kusaidia na kuunga mkono yaendelee, kumekuwa na mijadala mingi miongoni mwa Waislamu kuhusu jinsi ya kujihusisha zaidi kisiasa na jinsi jamii ya Kiislamu inavyoweza kuwa mstari wa mbele katika kuunda siasa za Marekani ili kubadilisha dunia kuwa bora. Ndani ya mijadala hii, mengi yanasemwa kuhusu kujishughulisha na uraia, kujiunga na kuunga mkono wagombea mahususi wa kisiasa, kunyima kura zao kama aina ya adhabu, na hatimaye kupata Waislamu zaidi, au "washirika" kwenye nyadhifa katika ngazi za dola na majimbo. Kuna gumzo hata miongoni mwa kina dada wakidai kwa furaha kwamba wanajaribu kumlea kijana au binti yao kuwa Rais wa kwanza wa Marekani Muislamu. Haya yanawekwa kama mafanikio sio tu kwa Waislamu wa Amerika, lakini Waislamu kote ulimwenguni. Huu unawekwa kama mpango wa mafanikio licha ya ukweli kwamba vyama vyote vya kisiasa, iwe vya rangi ya samawati, nyekundu, au kijani vinaunga mkono umbile la Kizayuni, au dola zengine zenye kufanya mauaji ya halaiki mithili ya China na India.