- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Je, Mafanikio kwa Waislamu yanaweza Kupatikana kupitia Siasa za Kidemokrasia?
(Imetafsiriwa)
Kutokana na mauaji makubwa ya halaiki yanayotokea Gaza na dori ya Marekani katika kusaidia na kuunga mkono yaendelee, kumekuwa na mijadala mingi miongoni mwa Waislamu kuhusu jinsi ya kujihusisha zaidi kisiasa na jinsi jamii ya Kiislamu inavyoweza kuwa mstari wa mbele katika kuunda siasa za Marekani ili kubadilisha dunia kuwa bora. Ndani ya mijadala hii, mengi yanasemwa kuhusu kujishughulisha na uraia, kujiunga na kuunga mkono wagombea mahususi wa kisiasa, kunyima kura zao kama aina ya adhabu, na hatimaye kupata Waislamu zaidi, au "washirika" kwenye nyadhifa katika ngazi za dola na majimbo. Kuna gumzo hata miongoni mwa kina dada wakidai kwa furaha kwamba wanajaribu kumlea kijana au binti yao kuwa Rais wa kwanza wa Marekani Muislamu. Haya yanawekwa kama mafanikio sio tu kwa Waislamu wa Amerika, lakini Waislamu kote ulimwenguni. Huu unawekwa kama mpango wa mafanikio licha ya ukweli kwamba vyama vyote vya kisiasa, iwe vya rangi ya samawati, nyekundu, au kijani vinaunga mkono umbile la Kizayuni, au dola zengine zenye kufanya mauaji ya halaiki mithili ya China na India.
Katika uchaguzi uliopita, baadhi ya Waislamu waliendelea kuwaunga mkono Wanademokrat licha ya uhalifu wao wa kivita huko Gaza kwa sababu walidai, "Waliberali ni washirika wetu." Baadhi ya Waislamu walimuunga mkono mgombea wa Chama cha Kijani, lakini walishindwa kutambua uungaji mkono wa chama hicho kwa dola ambazo pia zinafanya ukatili dhidi ya Waislamu nchini China na Urusi. Isitoshe, ukweli kwamba pia kilipuuza dori kuu ambayo umbile la Kizayuni linacheza katika sera za nje za Marekani na ahadi yoyote ya mgombea urais ya kuondoa uwepo wake haingii akilini. Hatimaye, kulikuwa na kundi la baadhi ya Waislamu waliomuunga mkono Trump kwa sababu walihisi angekomesha mauaji ya halaiki (na vita vyovyote vinavyoweza kutokea) na sera zake ni nzuri kwa Waislamu kifedha nchini Amerika. Ikiwa mgombeaji wako hakushinda, mtazamo uliopendekezwa ulikuwa kwamba, "tuna miaka 4 ya kufanya kazi katika kuunda KAMBI ya Waislam ya kupiga kura na kulenga kupata Waislamu wengi katika afisi za mitaa ili kupata uchaguzi ujao." Sababu na mikakati hii yote ilikuuzwa kama njia ya kupata mafanikio.
Je, uhalisia umekuwaje tangu Rais "aliye dhidi ya vita" aingie madarakani? Uhalisia umekuwa onyesho thabiti la kumuunga mkono Netanyahu na umbile la Kizayuni. Mabilioni zaidi yakitolewa kwa silaha kuendeleza unyakuzi wa ardhi, mateso, na mauaji ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Makamu wa Rais JD Vance akichochea hamasa ya kuchukia Uislamu katika safari yake ya hivi majuzi huko Ulaya, na hata ule unaoitwa usalama wa kifedha ambao Waislamu walihisi kuwa nao nchini Amerika unaondolewa polepole kwa kuondoa ufadhili kwa huduma ya Medicare/Medicaid na manufaa ya malipo ya uzeeni.
Ingawa ikhlasi ya Waislamu wa Marekani haitiliwi shaka, kwa vile pia wanaumia kutaka kukomesha mauaji ya halaiki na kukaliwa kwa mabavu Ardhi Iliyobarikiwa, ukweli usemwe, kupata mafanikio kama Ummah kamwe hakuwezi kutokea ikiwa tunatazama mfumo wa mwanadamu kutatua matatizo yetu na matatizo ya dunia. Mtume wetu Muhammad (saw) alikataa kujiunga na mfumo wa kisiasa wa Maquraish licha ya kuahidiwa utajiri na madaraka, na vilevile ahadi ya kukomesha unyanyasaji dhidi ya Waislamu wa Makka ili kusimamisha sheria za Mwenyezi Mungu (swt). Ingawa hili liliruhusu kuendelea kudhulumiwa kwake yeye (saw) na Waislamu, mihanga yao ilifungua njia kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuupatia Ummah ufanisi kwa kusimamisha Dola ya Khilafah na kuufanya ulimwengu wa Kiislamu kuwa nuru inayoongoza ulimwengu mzima. Dola na uongozi ulioongoza serikali iliyosimamia mambo ya raia wake na ilikuwa ndio kimbilio la wanyonge. Wema waliotangulia hawakuwa na mtazamo finyo, wasioona mbali, lakini walitazama picha kwa upana zaidi. Hawakuwa tu wakiangalia kupata manufaa na maslahi yao wenyewe, bali walijitolea mali, muda na maisha yao wenyewe ili kusimamisha dola ya Kiislamu mjini Madina, kama inavyofafanuliwa katika Serah.
Sisi kama Ummah tunatakiwa kuchukua msimamo huo. Tunapaswa kuangalia mbali na kushiriki katika mfumo wa wakandamizi wetu; waandaji wa ghasia zote, misukosuko, na umaskini kote ulimwenguni, na tufanye kama watangulizi wetu wema walivyofanya kwa kuangalia kuelekea kwenye Quran na Sunnah kama mwongozo wetu wa jinsi ya kubadili hali ya kisiasa. Kwa Waislamu nchini Amerika, hii ina maana ya kuangalia zaidi ya manufaa ya muda mfupi, kwani mara kwa mara tumeona mkakati huu ukifeli. Kwa Waislamu wa Marekani, hii ina maana kwamba ni lazima tuwe mstari wa mbele kutoa mfumo wa kisiasa wa Kiislamu kama suluhisho pekee la kutatua matatizo ambayo yanazidi kurundikana sio tu kwa Waislamu pekee, bali wanadamu wote. Ni lazima tuonyeshe uadilifu wa Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt) na jinsi utekelezaji wake kamili utakavyoleta utulivu na usalama kwa wale wanaoishi ndani ya mipaka yake mikubwa, iwe ni Waislamu, Wakristo, Mayahudi, Mabaniani, nk.
Kama vile Mtume wetu (saw) alivyofanya, sisi Waislamu lazima tufanye kazi kwa ajili ya kusimamisha tena mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) katika ardhi za Waislamu, ili kwamba kwa mara nyengine tena tupate kufaulu kwa Muumba wetu (swt) na kuwa nuru inayoongoza kwa ulimwengu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika