Ijumaa, 20 Shawwal 1446 | 2025/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tangazo la Matokeo ya Kuutafuta Mwezi Muandamo wa Shawwal 1446 H Pongezi kwa Idd Al-Fitr Iliyobarikiwa

Ummah umepitia mateso ya kubaki chini ya nira ya tawala za vibaraka. Umeshuhudia kwa macho yake wenyewe watawala wakifuja mali zake kwa makafiri, wakoloni wa Magharibi, kuzitelekeza kwao na sababu zake, kuzuia kwao majeshi kusonga ili kuinusuru Palestina kutoka kwenye makucha ya Mayahudi wahalifu, uingiliaji wa wazi wa Magharibi katika dini yake na uadilifu wake, na jaribio la kuulazimisha kulishuhudia  umbile la Kiyahudi, na kuuacha na chaguo kati ya uhalalalishaji mahusiano au kifo. Mandhari na matukio haya yote yameufanya utambue kwamba bila ya utawala wa Uislamu, utabakia kukoloniwa, kulengwa, na kudhalilishwa. Kukinaika kwake kwa haja ya dola ya Khilafah kumeimarishwa, na kwa hakika, Khilafah imekuwa ni kiu yake.

Soma zaidi...

Enyi Majeshi: Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache

Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu, hasa zile zinazoizunguka Palestina: Je, kuna udhuru wowote uliobaki kwa wanaoomba msamaha? Je, kuna hoja yoyote iliyobaki kwa wanaolaani? Vipi mnaweza kuona na kusikia uvamizi na mauaji ya Mayahudi hali mmekaa katika sehemu zenu, bila kutikisika, badala ya kuelekea katika ardhi ya Al-Ribat, Palestine Ardhi Iliyobarikiwa, ili kurudisha uvamizi wa Mayahudi na kuliondoa umbile lao?

Soma zaidi...

Trump na Mfuasi wako Netanyahu: Macho Yako Yamepofushwa

“Mapema leo, Rais Trump wa Marekani alithibitisha mpango wake wa Marekani kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwafukuza Wapalestina, akisema kwamba amejitolea kuinunua na kuimiliki Gaza. Kauli hii ilitolewa na Trump mnamo Jumapili jioni ndani ya ndege ya Air Force One alipokuwa akielekea New Orleans kuhudhuria Super Bowl." (BBC, 10/2/2025) Baadaye, wakati wa mkutano wake na Mfalme wa Jordan, alisema: "Wapalestina wataishi kwa usalama mahali pengine, nje ya Gaza, na ninaelewa kwamba tuna uwezo wa kufikia suluhisho,"

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu