Jibu la Swali: Kuongezeka kwa Uhasama nchini Sudan
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Al Arabiya Net ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo tarehe 4/2/2025: "Jeshi na vikosi vyake vya usaidizi viliingia katika maeneo ya kusini-mashariki ya Jimbo la Khartoum wakati wa saa zilizopita, wakitokea Jimbo la Al-Jazeera.." na tovuti ya Youm7 ilichapishwa mnamo tarehe 2/2/2025: "Mwandishi wa Kituo cha Habari cha Cairo aliripoti katika habari mpya zinazochipuka kwamba jeshi la Sudan linachukua idadi kadhaa ya vijiji mashariki mwa mto Nile katika Jimbo la Khartoum." Kabla ya hapo, mnamo tarehe 11/ 1/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka vilishindwa na jeshi la Sudan katika mhimili wa Jimbo la Al-Jazeera na mji mkuu wake, Wad Madani, “na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Hemeti, alikiri katika kanda ya sauti iliyohusishwa naye kwamba vikosi vyake vilishindwa katika Jimbo la Al-Jazeera...” (Al-Jazeera 1/13/2025).