Amerika inaharakisha Mpango wake wa Kulitenganisha Eneo la Darfur Hakuna Suluhisho Isipokuwa kwa Kuufanya Umoja wa Dola kuwa Suala Nyeti
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tangu utawala wa Trump kuchukua faili ya Sudan baada ya kuchukua uongozi mnamo Januari 2025, imekuwa ikiongoza harakati za kijeshi na kisiasa nchini Sudan, ikishinikiza kujitenga kwa eneo la Darfur. Mnamo Jumatano, 26/3/2025, jeshi liliteka tena Khartoum. Al-Burhan alitangaza kutoka Kasri la Republican, “Khartoum iko huru na suala limekwisha.” Hatua za kijeshi ziliharakisha, na kuondoa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kutoka Sudan ya kati, ikijumuisha majimbo ya Al-Jazirah, Sennar, White Nile na Blue Nile.