Enyi Wanajeshi wa Misri (Kinana): Vivuko vya Gaza havihitaji Malori, Bali vinahitaji Majeshi na Magari ya Kivita
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hali ya kibinadamu mjini Gaza imefikia viwango vya maafa ambavyo havijawahi kushuhudiwa. Idadi ya vifo vya mashahidi imezidi 65,000. Ripoti za kimataifa zinaweka idadi hiyo kuwa 40% zaidi. Hao ni zaidi ya mashahidi 100,000 na takriban wakimbizi wa ndani milioni 1.9, ambao ni karibu asilimia 90 ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza, ambao wanaishi katika mazingira yasiyo ya kibinadamu, na kunyimwa mahitaji ya kimsingi ya maisha. Gaza inakabiliwa na njaa ya kweli, haswa katika sehemu ya kaskazini ya Ukanda huo. Hospitali zinafanya kazi chini ya 30% ya uwezo wao, na uhaba wa dawa na mafuta unaweka makumi ya maelfu ya wagonjwa katika hatari ya kifo cha polepole. Takwimu hizi zinafichua ukubwa wa maafa hayo na kuthibitisha kuwa kinachoendelea ni vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Gaza.