Sio Kumwasilisha Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah, kwenye Mahakama Yoyote, Hata Baada ya Miaka Kumi na Moja, Wala Kumwachilia Huru, Kunathibitisha Uthabiti wa Naveed Butt, na Batili na Uoga wa Watawala
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 11 Mei 2023, imekuwa ni miaka kumi na moja tangu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, Naveed Butt, kutekwa nyara na asasi za serikali. Naveed Butt alitekwa nyara na majambazi wa serikali katika jiji la Lahore, mnamo tarehe 11 Mei 2012, alipokuwa karibu kuregea nyumbani, baada ya kuwachukua watoto wake shuleni.