Barua ya Wazi kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia kwa Wajumbe wa Serikali ya Tunisia Kutia saini Mkataba na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni Ala Nyingine ya Ukoloni kwa Tunisia
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya makubaliano ya mnamo tarehe 15 Oktoba 2022 kati ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Tunisia katika ngazi ya wataalamu wa ufadhili wa dolari bilioni 1.9 kwa kipindi cha miaka 4, sisi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, tunawahutubia, tukiwashauri na kuwaonya juu ya matokeo ya mkataba huu na madhara yake kwa nchi na wananchi, hasa kwa vile mumedai, kwa zaidi ya mara moja, kwamba mumekuja kurekebisha yale yaliyofisidiwa na serikali zilizopita!