Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Barua ya Wazi kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia kwa Wajumbe wa Serikali ya Tunisia

Kutia saini Mkataba na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni Ala Nyingine ya Ukoloni kwa Tunisia
(Imetafsiriwa)

Mabibi na Mabwana, Wajumbe wa Serikali ya Tunisia

Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

Baada ya makubaliano ya mnamo tarehe 15 Oktoba 2022 kati ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Tunisia katika ngazi ya wataalamu wa ufadhili wa dolari bilioni 1.9 kwa kipindi cha miaka 4, sisi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, tunawahutubia, tukiwashauri na kuwaonya juu ya matokeo ya mkataba huu na madhara yake kwa nchi na wananchi, hasa kwa vile mumedai, kwa zaidi ya mara moja, kwamba mumekuja kurekebisha yale yaliyofisidiwa na serikali zilizopita!

Mabibi na Mabwana,

Serikali za kabla ya mapinduzi na baada ya mapinduzi zilitabanni sera ya kukopa ili kukabiliana na migogoro ya kiuchumi na kutoa ahadi za kutekeleza mipango ya nje na kuamuru bila kutaja sababu halisi zilizosababisha kutumbukia katika mzunguko wa madeni na kuingiza uchumi katika hali mbaya ambayo mahitaji ya serikali ya mikopo yanaongezeka ili kulipa madeni ya awali, pamoja na kuwachosha wananchi kwa kuongeza kodi za kidhulma zenye kutawanyika, hasa kwa wakopeshaji wa kigeni.

Bila shaka, munafahamu kuwa mikopo iliyotolewa kwa Tunisia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) mwaka 2013 (dolari bilioni 1.5), 2016 (dolari bilioni 2.8) na 2020 (dolari bilioni 0.745) haikutatua tatizo la kiuchumi. Kinyume chake, umaskini umeongezeka na kuongezeka, ukosefu wa ajira, mfumko wa bei, na madeni yameongezeka kwa kasi kutokana na mikopo na ulipaji madeni (riba) na kuzorota kwa bei ya sarafu, hadi kufikia dinari bilioni 114, kulingana na utabiri wa Wizara ya Fedha kwa mwaka huu (2022).

Jambo la hatari zaidi ni kwamba zaidi ya theluthi mbili ya madeni haya yanadaiwa na vyama vya nje ambavyo hubadilisha ada zao za kifedha kwa masharti ya kidhulma, ambapo IMF ilitumia mikopo kama chombo cha kulazimisha masharti yake kwa Tunisia, kama vile kupunguza wingi wa mishahara, kuondoa ruzuku kwa kawi na vyakula msingi, kupunguza thamani ya dinari, kubana matumizi ya serikali, kuongeza kodi, kubinafsisha mali ya umma na kuwapa wageni, na kuingiliwa kwa sheria, nyanja ya kitamaduni, na kisiasa, na utegemezi na uzorotaji wa kisiasa kwa kiwango cha maisha na maadili ya jamii. Katika suala hili, inatosha kuregelea Sheria ya Uwekezaji na Sheria ya Uhuru wa Benki Kuu ili kujua kiwango cha maafa yaliyosababishwa na kile kinachoitwa mageuzi makubwa yaliyowekwa na IMF na Umoja wa Ulaya kwa serikali iliyopita ya Youssef Chahed.

Mnajua kuwa masharti ya IMF hayafanyiwi mazungumzo au kujadiliwa, na inaweza kuruhusu serikali kuchukua muda wa kutekeleza masharti yake, lakini hairuhusiwi kuyabadilisha hata kidogo, na kama ushahidi, iligoma mwaka 2019 kuikabidhi Tunisia awamu ya sita na saba ya mkopo ulioongezwa muda (2016-2020), licha ya utekelezaji wa asilimia 85 ya masharti ya mkopo wa kile kinachoitwa marekebisho (dictions) hitajika, kulingana na kile kilichoelezwa. na Tawfiq Al-Rajhi, waziri wa zamani anayehusika na mageuzi makubwa, ambayo inathibitisha kwamba kazi kuu ya IMF duniani ni kupanua ushawishi kupitia masharti inayolazimisha nchi.

Mabini na Mabwana,

Je, munatarajia, kwa kutabanni sera ya ukopaji, kuwa na matokeo tofauti na ya watangulizi wenu waliokuwa madarakani?

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inatambua kwamba munafahamu madhara makubwa ya masharti haya, kama inavyothibitishwa na ukweli kwamba mulifanya makubaliano ya kuongeza mishahara na Muungano Mkuu wa Wafanyikazi wa Tunisia, kwa upande mmoja, ili kuzima hasira za mitaani, na kwa upande mwingine, kwa mjibu wa IMF, ambayo iliweka maelewano na muungano huo ili masharti yake yatekelezwe bila usumbufu.

Mikopo ya nje ina madhara ya kihakika kwa uhuru wa nchi na uamuzi wa kisiasa. Njia ya mikopo ya nje kwa ajili ya kufadhili hapo awali ilikuwa njia ya ukoloni wa moja kwa moja wa nchi. Kupitia hilo, Wafaransa walikuja kuitawala Tunisia, na leo hii ni njia ya msingi ya kupanua ushawishi na njama dhidi ya nchi hiyo, na hakuna wema wowote unaotoka humo. Nchi yetu, Tunisia, ndiyo shahidi bora wa hili. Jumla ya deni la umma kwa dinari lilifikia dinari bilioni 105.7 Machi iliyopita, ikimaanisha kuwa liliongezeka maradufu kwa zaidi ya mara 4 kuliko ilivyokuwa mwaka 2010 (dinari bilioni 25).

Hivi kwa kukopa kutoka IMF ya kikoloni, je mtakatiza sera za waliokutangulia madarakani, na kurekebisha walichochafua? Au mutakusanya deni la Tunisia zaidi na zaidi na badali yake kuuweka rehani uwezo wa kiuchumi wa nchi, uamuzi wake wa kisiasa, na mustakabali wa vizazi vijavyo kwa adui mjanja ambaye anaendelea tu kutuangalia?

Mabibi na Mabwana,

Uchumi haushughulikiwi kupitia kukopa kutoka kwa shirika hili la kimataifa au lile, lakini kupitia kusimama juu ya ulisia wa tatizo la kiuchumi tangu mwanzo na kutafuta tiba sahihi, haswa kwa kuwa mzozo wa kiuchumi nchini Tunisia sio mgogoro wa muda mfupi, bali ni mgogoro wa kimuundo unaojumuisha sekta zote za kiuchumi, na sababu yake kuu ni mfumo wa kirasilimali ambao uliwezeshwa, kupitia sheria zake za kiuchumi, kuweka uchumi wa nchi chini ya utawala wa Magharibi na zana zake za kifedha, ambapo ilipelekea:

- Kulazimisha sera tasa za kiuchumi chini ya kichwa cha mageuzi ya kiuchumi ambayo taasisi za fedha huhitaji wakati wa kutoa mikopo, ambazo zilizuia sekta muhimu kama vile kilimo, viwanda na biashara, na kuzibadilisha sekta za pambizoni kama vile utalii. Na ulazimishwaji wa Makubaliano Shirikishi pamoja na Muungano wa Ulaya, ambayo yaliangamiza muundo wa viwanda, kuongeza viwango vya ukosefu wa ajira na viwango vya umaskini, na kuongeza nakisi ya biashara.

- Kunyakuliwa kwa taasisi za umma na kuporwa kwa utajiri wa nchi wa mafuta, gesi, madini na mengineyo na makampuni ya kikoloni kwa jina la uwekezaji kutoka nje.

- Kuunganisha dinari kwa fedha za kigeni, na kusababisha thamani yake kushuka karibu hadi kuipoteza. Dinari ya Tunisia ilishuka thamani dhidi ya dolari wakati wa miaka iliyofuata mapinduzi kwa 128% (dinari 1.42 kwa dolari mwaka 2011 hadi dinari 3.25 kwa sasa).

Zaidi ya hayo, mfumo wenyewe wa kibepari ndio shina la ugonjwa na adha mbaya zaidi kwa sababu misingi ambayo maisha ya uchumi wa kibepari yamejengwa juu yake kimaumbile ni haribifu. Miongoni mwa fikra hizi za kibepari zenye uharibifu na fahamu hatari za kiuchumi ni:

- Kuonyesha tatizo la kiuchumi kama uhaba wa bidhaa na huduma (utajiri), na sio ugavi adilifu wa utajiri huu.

- Utegemezi wa uchumi wa kibepari juu ya riba.

- Ufisadi wa mfumo wa fedha duniani, ambao uliondoa dhahabu na fedha kutoka kwa pesa taslimu, na kuifanya dolari kuwa ndio msingi wa pesa za kimataifa.

- Udhibiti wa kimakosa wa mali ambayo imegawanywa katika sekta binafsi (mali binafsi) na sekta ya umma (umiliki wa dola), na kuacha umiliki wa umma ambao Uislamu uliainisha na kuutofautisha na mifumo mingine.

Kilichofanya mambo kuwa mabaya zaidi ni kwamba ubepari uligeuzwa na kuwa mfumo lazimishi wa kiulimwengu chini ya jina la utandawazi, ambapo ulisababisha kuongezeka kwa hali mbaya ya uchumi wa dunia na athari za haraka za migogoro katika uchumi dhaifu wa nchi, kama inavyotokea leo nchini Tunisia, kwa mfano, kiwango cha juu cha mfumko wa bei, mtikisiko wa sarafu na kuenea kwa umaskini uliokithiri kutokana na Virusi vya Korona na vita kati ya Urusi na Ukraine

Mabibi na Mabwana,

Barua yetu hii ni mwaliko wa dhati uliotumwa na Hizb ut Tahrir kwa wajumbe wa serikali, ili kukata mafungamano yao na taasisi za fedha za kimataifa na wasikubali maagizo ya IMF na dozi zake hatari, kwa sababu inaamiliana na riba, ambayo imeharamishwa na Sharia, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

(يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ)

“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.” [Al-Baqarah 2:276]. Na maneno ya Mwenyezi Mungu: (وَأَحَلَّ اللهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا)  “Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.” [Al-Baqarah 2:275].

Hatari zaidi katika suala hilo ni kwamba mamlaka na wataalamu wake, wahitimu wa shule ya kibepari, wanasisitiza juu ya kuunganisha Tunisia na Magharibi na kuutenga Uislamu na hukmu zake. Karne kumi na tatu, misafara ya zakat ilikuwa ikizunguka nchi nzima kutafuta maskini mmoja wa kuchukua zakat, lakini hapakuwa na yeyote, huku umaskini leo unajumuisha karibu kila mtu isipokuwa kwa wadau wachache.

Hivyo basi, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunakualikeni kuachana na kanuni ya kibepari na mfumo wake wa kiuchumi na kifedha, kukataa kujibu mashinikizo ya kimataifa na kukataa misaada ya kimataifa na mikopo ya benki, na badala yake lazima muchangamshe mradi wa kihadhara wa Kiislamu ili muweza kutazamia maisha mapya, salama na amani yasiyo na migogoro ya kiuchumi au kifedha, kwa kuzingatia uadilifu wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Uislamu uliweka mfumo wa kiwahyi unaozuia tabaka lolote katika jamii kuwadhibiti watu wengine wote.

Mabibi na Mabwana,

Kutabanni Uislamu kama kanuni ambayo kwayo mfumo unachipuza, utekelezaji wa mifumo yake, ukiwemo mfumo wa kiuchumi, inatosha kutatua matatizo na migogoro yetu. Misingi ambayo Uislamu uliweka sheria na juu yake ukajenga mfumo wake wa kiuchumi ina uwezo wa kipekee wa kutatua matatizo ya kiuchumi nchini bila ya haja ya kukopa kutoka katika taasisi za fedha za kimataifa za kikoloni ambazo hazitaki sisi kuinuka wala kunyanyuka, na misingi hii inatosha kugawanya upya mali katika mgawanyo wa kiadilifu katika mujtamaa, hivyo hakuna mtu anayemdhibiti mtu yeyote na matajiri wachache na makampuni machache ya kigeni hawadhibiti rasilimali za nchi na watu.

Suluhu hizi si za kindoto, bali ni fikra inayoshughulikia na uhalisia, na zilikwisha tumika katika historia ya Kiislamu katika zama za Khilafah, na zilitoa kheri kubwa, na jambo hili litaregea tena, Mwenyezi Mungu akipenda, kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyotaja katika Hadith sahih:

«يَكُونُ فِي آخِرِ أُمَّتِي خَلِيفَةٌ يَحْثِي الْمَالَ حَثْياً، لَا يَعُدُّهُ عَدَداً»

Mwishoni mwa Ummah wangu kutakuwa na Khalifa ambaye atahimiza mali kisawa sawa, lakini hataihesabu kwa idadi.” (Imepokewa na Muslim).

H. 28 Rabi' I 1444
M. : Jumatatu, 24 Oktoba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu