Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 27 Safar 1447 | Na: H.T.L 1447 / 02 |
M. Alhamisi, 21 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Usaliti Mpya: Mamlaka ya Lebanon Yamwachilia Huru Mmoja wa Wafungwa Wanaohusishwa na umbile la Kiyahudi!
(Imetafsiriwa)
Leo, Alhamisi, tarehe 21/8/2025, mamlaka ya Lebanon ilimwachia huru ghafla Saleh Abu Hussein, ambaye ni mmoja wa washirika wa umbile la Kiyahudi, bila kubadilishana na yeyote! Na wakamkabidhi kwa umbile hilo kililokuwa mstari wa mbele wa ukaliaji kimabavu wa Palestina mjini Naqoura!
Taarifa hii inakuja baada ya ziara ya wajumbe wa Marekani Barrak na Ortagus nchini Lebanon! Katika wakati ambapo umbile la Kiyahudi linaendelea kuua, kupiga makombora na kuharibu miji na vijiji vyote vya Lebanon, na kuwatia jela watu wengi wa Lebanon, na kuvikalia kwa mabavu vijiji vingi vinavyopakana na Palestina, pamoja na mauaji yake mjini Gaza na Ukingo wa Magharibi.
Kitendo hiki cha khiyana cha kutojali cha mamlaka hii ni jinai kwa maana ya kisheria na kisiasa, na kushirikiana na kujisalimisha kwa amri za Marekani na Mayahudi, bali pia ni jinai katika maana ya kisheria, kama sheria inavyoeleza kuwa umbile la Kiyahudi ni adui na mvamizi, basi vipi jasusi mwenye uhusiano nalo, ambaye aliingia kwa kunyemelea, aachiliwe huru bila ya uamuzi wowote wa kimahakama na bila hoja yoyote ya kisheria?!
Lakini haishangazi, kwani usaliti huu ulitanguliwa na usaliti katika kuwaachilia huru vibaraka wa uhalifu wa Mayahudi, hata wale ambao walimwaga damu nyingi za watu wa Lebanon, wakijua kwamba mamlaka nchini Lebanon inaendelea wakati huo huo kuwekwa kizuizini kisiasa mamia ya watu, na kuwaandama maelfu ya watu wasio na hatia, chini ya mashtaka ya uwongo ya ugaidi, na kuunga mkono mapinduzi ya al-Sham kwa muda wa miaka kumi na zaidi bila ya kufikishwa mahakamani, katika unyanyasaji ulio wazi kutoka kwake dhidi ya hadhi ya watu wake na watu wa Syria. Mamlaka ambayo Waziri Mkuu wake Salam hivi karibuni alishika wadhifa wa jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya “Haki” kwa muda wa miaka tisa, na rais wake iliahidi kukomesha kesi hizi za dhulma, kwa hiyo je kuachiliwa huru kwa jasusi huyo kumekuwa muhimu zaidi kuliko kuachiliwa huru kwa wasio na hatia?!
Ingefaa zaidi kwa mamlaka hii kuharakisha kuwaachilia huru watu hawa, kuwafidia madhara yaliyowapata, na kuwaadhibu madhalimu wao.
Sisi katika Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon tunakumbusha:
Kwamba mamlaka nchini Lebanon ni upanuzi wa mamlaka zilizowekwa katika ardhi za Waislamu, nazo ni mamlaka zisizo na uhalali na zilizo tiifu kwa Magharibi kafiri na zana zake katika ardhi zetu, ambazo zinajali tu maslahi ya Magharibi na kutekeleza amri zake kwa gharama ya maslahi ya watu na uangalizi wao, bila ya kuzingatia hata kidogo maadili, imani, na hukmu.
Enyi watu wa Lebanon na wakaazi wake kutoka katika nchi jirani, msitarajie uadilifu kutoka kwa mamlaka hii, wala uchungaji wala kujali, na yakinisheni kwamba suluhisho la Lebanon ni kuirudisha kwenye asili yake, kama sehemu ya ardhi ya ash-Sham chini ya kivuli cha Khilafah Rashida ambayo inasimamia mambo yenu, inaondoa dhulma kwenu, inaregesha haki kwa wamiliki wake, inazuia nchi za Magharibi kutokana na uingiliaji mambo wake, inalifagilia mbali umbile la Kiyahudi, inazuia khiyana, na kuharamisha usaliti, kwani ni ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo itatimia hivi karibuni, na kwayo tunaifanyia kazi.
[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً]
“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |