Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 2 Rabi' I 1447 | Na: H.T.L 1447 / 03 |
M. Jumatatu, 25 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon
Wamtembelea Meya wa Sidon
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon, uliowakilishwa na Kamati ya Shughuli katika Eneo la Kusini na Kamati Kuu ya Mawasiliano, ulifanya ziara ya kumkaribisha Meya wa Sidon, Mheshimiwa Mhandisi Mustafa Hijazi, mnamo Jumatatu tarehe 25/8/2025.
Ujumbe huo ulielezwa kwa mukhtasari maono ya manispaa na matatizo yanayoikabili katika kuregesha na kuwezesha kazi zake, na katika kufufua na kuamsha mapato ya manispaa kutoka kwa huduma zake husika.
Mambo kadhaa ya kila siku yanayohusiana na kazi ya manispaa ya jiji yalijadiliwa.
Ujumbe huo uliashiria haja ya kuhifadhiwa kitambulisho cha mji wa Sidon kwa kuzingatia mabadiliko na mazingira magumu yanayoizunguka Lebanon na kanda hii. Ujumbe huo ulipokea maoni chanya kuhusu suala hili kutoka kwa Meya.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |