Mzunguko wa Migogoro ni Lazima Ukome kwa Umma
- Imepeperushwa katika Siasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ummah umekuwa katika mzunguko wa migogoro kwa miaka 105. Mzunguko wa migogoro ambao umeathiri Ummah ni ule ambao umekuwa wa kimakusudi na wenye shabaha katika kusababisha aina mbalimbali za ukandamizaji na mateso kwa watu na mazingira. Leo, tunashuhudia mauaji kadhaa ya halaiki: Gaza na Palestina, Kashmir, Turkistan Mashariki, Sudan, na vitendo vya vurugu vya kudumu nchini Nigeria, Ethiopia, Syria, Lebanon, Congo, na Venezuela. Orodha hii inaweza kuendelea kwa sababu kila siku mji au nchi mpya inasogezwa karibu na janga kubwa na Magharibi ya kikoloni, yaani Amerika, ambayo hupora na kuyumbisha nchi baada ya nchi ili kuhakikisha kwamba udhibiti wake unabaki imara.



