Mkutano wa SCO jijini Islamabad: Siasa za Jiografia ndani ya Kivuli cha Uhasimu wa Marekani na China
- Imepeperushwa katika Siasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya ulinzi mkali jijini Islamabad, Mkutano wa 23 wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) ulianza kwa kishindo cha kawaida. Mkutano huo uliohudhuriwa na dola zenye nguvu kama China, Urusi, India, Pakistan, Iran na baadhi ya jamhuri za Asia ya Kati, ulimalizika kwa kutiwa saini hati nane, zinazohusu bajeti ya shirika hilo, shughuli za sekretarieti ya SCO, na juhudi za kukabiliana na ugaidi katika kanda. Jambo kuu lililoangaziwa lilikuwa ni kuidhinishwa kwa China kama Mwenyekiti kwa kipindi cha 2024-2025.