Msimamo kwa Sherehe za Maadhimisho ya Mapinduzi Mawili ya Septemba Moja yaliingiza Usekula nchini Yemen na Mengine Yalitoa Wito wa Kuuimarisha!
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika mwezi wa Septemba wa kila mwaka Yemen ina matukio mawili; la kwanza mnamo tarehe 26 Septemba 1962 ambayo ni kumbukumbu ya kupinduliwa kwa mfumo wa kifalme nchini Yemen Kaskazini, na la pili mnamo tarehe 21 Septemba 2014 ambayo ni kumbukumbu ya kuingia kwa Mahouthi jijini Sana’a ambayo ilisababisha udhibiti wao wa mikoa ya kaskazini.