Vitisho vya Kutojali vya Trump Vitasambaratishwa dhidi ya Mwamba wa Ustahamilivu wa Gaza
- Imepeperushwa katika Iraq
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mara tu Trump alipotwaa urais wa Marekani, alianza kutoa vitisho kushoto na kulia. La kukasirisha zaidi kati ya haya lilikuwa ni tangazo lake la nia yake ya kuwahamisha kwa nguvu watu wa Gaza. Alisisitiza tena uungaji mkono wake wa kufukuzwa kwa kudumu kwa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza hadi nchi nyingine wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi mnamo Jumanne, 4 Februari 2025. Hata alitangaza nia yake ya kununua ardhi ya Gaza na kuigeuza kuwa mradi wa uwekezaji!