Jumamosi, 23 Sha'aban 1446 | 2025/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  12 Sha'aban 1446 Na: 1446 / 08
M.  Jumanne, 11 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vitisho vya Kutojali vya Trump Vitasambaratishwa dhidi ya Mwamba wa Ustahamilivu wa Gaza
(Imetafsiriwa)

Mara tu Trump alipotwaa urais wa Marekani, alianza kutoa vitisho kushoto na kulia. La kukasirisha zaidi kati ya haya lilikuwa ni tangazo lake la nia yake ya kuwahamisha kwa nguvu watu wa Gaza. Alisisitiza tena uungaji mkono wake wa kufukuzwa kwa kudumu kwa Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza hadi nchi nyingine wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi mnamo Jumanne, 4 Februari 2025. Hata alitangaza nia yake ya kununua ardhi ya Gaza na kuigeuza kuwa mradi wa uwekezaji! Alisisitiza msimamo huo wakati wa mkutano wake na msaliti wa Jordan, akidai kuwa suluhisho la mzozo huo linatokana na kuondoka kwa Wapalestina kutoka Gaza, akipendekeza kuwa nchi zingine isipokuwa Jordan na Misri zitakuwa tayari kuwapokea. Aliongeza kuwa anataka watu wa Gaza watafute mahali pazuri pa kuishi kwa sababu kinachoendelea kwenye mahandaki hayo na kwengineko ni machafuko, na akaendelea kusema kuwa "watu wa Gaza hawajui chochote ila kifo na uharibifu."

Ingawa kauli zake zilimgeuza kuwa kinyago na kukabiliwa na kukataliwa na Wapalestina, Waarabu na kimataifa, huku magazeti ya kimataifa yakiita mapendekezo yake kuwa ya ajabu na hatari, aliendelea na vitisho vyake. Mnamo Jumatatu, 10 Februari 2025, alitangaza: "Ikiwa mateka wote hawatarudishwa kutoka Gaza kufikia saa 12:00 adhuhuri mnamo Jumamosi, nitatoa wito wa kubatilishwa kwa usitishaji vita."

Mtu huyu mwehu anashindwa kutambua kwamba mikwala na vitisho vyake vinafanya kazi tu kwa vibaraka waoga ambao wameuza Ummah wao kwa ajili ya madaraka na vyeo vinavyodhibitiwa na mabwana zao— wale ambao Mwenyezi Mungu Anawaeleza: [إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ] “Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake.” [Aal-i-Imran:175]

Lakini vitisho hivyo havina uzito kwa wale waliojitolea nafsi zao kwa Mwenyezi Mungu na wakayafanya mapambano yao kuwa ni uhai na kifo, wakitafuta ima Nasr (ushindi) au kifo cha kishahidi. Ushahidi wa hili ni miezi kumi na tano ya vita ambayo Gaza imevumilia mikononi mwa adui wa Kiyahudi.

Watu wasio na silaha wa Gaza, pamoja na mujahidina, walisimama kidete dhidi ya uvamizi wa kikatili na uhalifu wa kutisha ambao ulilenga watu, miti, na mawe. Umbile la Kiyahudi lilitumia kila njia ya uhalifu iliyokuwa nayo, ikiungwa mkono na Amerika na Magharibi, huku watawala wa Waislamu wakiwasaliti watu wao na majeshi yao yakitulia tuli ndani ya kambi zao. Licha ya yote hayo, walishindwa kuwakomboa mateka wao!

Je, rais wa Marekani sasa anajaribu, kupitia kauli zake, kuupurukusha ulimwengu kutokana na kushindwa kwa Mayahudi mikononi mwa kundi dogo lakini lenye imani?

Je, hakushuhudia kwa macho yake makumi ya maelfu ya Wapalestina waliokimbia makaazi yao wakiregea kaskazini mwa Gaza, licha ya kutokuwa na makaazi, wakikwamia ardhi yao bila kujali kafara yoyote?Au macho yake yamezibwa?

Enyi Waislamu, enyi watu wa uongofu na wema!

Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa vimefichua na kuwafichua wengi, na kuugawanya Ummah katika kambi mbili na sio tatu: Kambi ya wale wanaosimama imara juu ya haki, kama alivyobashiri Mtume (saw), ambaye alisema kwamba hakuna madhara yoyote yatakayowapata kutoka kwa wale wanaowasaliti. Na kambi ya batili inayoongozwa na wanafiki wanaowatelekeza watu wa haki na kutanguliza utawala wa madhalimu juu ya utawala wa Mwenyezi Mungu.

Enyi Majeshi ya Umma wa Kiislamu!

Watu wa Gaza wamebaki imara katika uvamizi huu wote, wakiuthibitishia ulimwengu—na kwenu—wajibu ulio juu ya mabega yenu. Mwenyezi Mungu atakuulizeni juu ya kila tone la damu ya Waislamu iliyomwagika katika Ardhi hii Iliyobarikiwa. Je, mutawatelekeza na kuwaacha wakabiliane na njama ovu za Marekani na Mayahudi peke yao? Au je, mtatii wito wa Mwenyezi Mungu, kuvivunja viti vya utawala vya wasaliti, na mtembee kuikomboa Gaza na ardhi yote ya Al-Isra na Al-Mi’raj kutokana na uchafu wa Mayahudi?

Hizb ut Tahrir inakuombeni muinuke kwenye heshima hii kubwa na wajibu mkubwa—kuwa Maanswari (wasaidizi) wa Mwenyezi Mungu. Je, mutaitikia wito?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu