Umbile la Kigaidi la Kizayuni Limeufanya Ukingo wa Magharibi kuwa Makaburi ya Watoto kama vile Gaza, Huku Majeshi ya Nchi za Waislamu Yakitazama
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 7 Februari, shirika la ‘Save the Children’ liliripoti kwamba watoto wasiopungua 224 wameuawa katika Ukingo wa Magharibi na wanajeshi au walowezi wa Kizayuni tangu Januari 2023, mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 2 pekee. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 171 waliuawa katika Ukingo wa Magharibi tangu tarehe 7 Oktoba 2023 - sawia na karibu 1 kila siku. Hakuna mwanajeshi wa Kizayuni aliyefunguliwa mashtaka au kuwajibika kwa mauaji haya. Afisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ilisema kuwa kumekuwa na ongezeko la mara 20 la idadi ya watoto wa Kipalestina waliouawa na mashambulizi ya anga ya umbile la Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi katika miaka ya hivi karibuni.