Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan: Gaza inahitaji kuingia kwa majeshi ya Waislamu, sio tu misaada ya kibinadamu!
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Taarifa ya mwisho ya Mkutano wa Waarabu, ulioandaliwa na mji mkuu wa Iraq, Baghdad mnamo tarehe 17 Mei 2025, ilisisitiza haja ya kuleta misaada ya kibinadamu mjini Gaza. Watawala wa Waislamu, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, wamezuia majeshi ya Waislamu kupigana na Mayahudi, kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu. Mtume ﷺ ametuambia kuwa kupigana na Mayahudi na kuwashinda kunaleta malipo makubwa.