Mazoezi ya Phoenix Express 2025 Sura Nyingine katika Sura za Utiifu kwa Utawala wa Marekani
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Maandalizi ya Tunisia kuandaa toleo jipya la mazoezi ya kijeshi ya pande nyingi, Phoenix Express 2025, katika mwezi huu wa Novemba yanakuja, na hili ndilo zoezi ambalo Komandi ya Marekani ya Afrika imeanza kuandaa kila mwaka baada ya mamlaka iliyopo sasa nchini Tunisia kuihusisha nchi yetu kwa kutia saini pamoja na Marekani, mnamo tarehe 30/09/2020, makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi, ambayo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper aliyataja kama ramani ya utendakazi inayoendelea kwa miaka kumi.



