Ijumaa, 10 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muasisi wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Mwanachuoni Taqiuddin an-Nabahani

(rahimahu Allah)

Taqiuddin bin Ibrahim bin Mustafa bin Ismail bin Yusuf an-Nabahani (muasisi wa Hizb ut Tahrir) anatoka katika kabila la Bani Nabahan na anatoka kijiji cha Ajzam mji wa Haifa eneo la Kaskazini mwa Palestina. Sheikh an-Nabahani alizaliwa katika kijiji cha Ajzam mnamo 1332 Hijria au 1914 Miladi. Familia yake ilijulikana kwa ilimu, kushikamana na Dini na Uchamungu. Babake, Sheikh Ibrahim, alikuwa ni faqihi na mwanachuoni wa ‘Uloom e Sharai’ katika Wizara ya Ma'arif (Ilimu na Sanaa). Mamake naye alikuwa ni mjuzi katika ‘Uloom e Sharai,' aliyoipata kutoka kwa babake Sheikh Yusuf an-Nabahani.

Riwaya tofauti tofauti zimemtaja babu yake mzalia mamake Sheikh Yusuf Nabahani kwa maneno haya: Yusuf bin Ismail bin Yusuf bin Hassan bin Mohammad Al Nabahani Al Shafii’ – kunya yake (jina la lakabu) ilikuwa ‘Abu al Mahasin’ na alikuwa mshairi, Sufi na msomi. Alichukuliwa kuwa miongoni mwa makadhi wazuri zaidi wa zama zake. Alihudumu kama kadhi katika eneo la Jenin lililounganishwa na Nablus. Baadaye, alihamia Istanbul ambako alihudumu kama kadhi katika eneo la Kavi Sanjaq mjini Mosul. Hatimaye aliteuliwa kama mkuu wa mahakama ya kifalme eneo la Al-Azqya na Al-Quds. Na kisha alichukua usimamizi wa Mahakama ya Haki ya Beirut. Ameandika vitabu arubaini na nane.

Shakhsiyya (Utambulisho) ya Kiislamu ya Sheikh Taqiuddin kwa kiwango kikubwa ni athari ya msingi wa familia yake. Hivyo basi, alihifadhi Qur’an Tukufu akiwa na umri wa miaka 13. Alivutiwa sana na ilimu na utambuzi wa babu yake mzalia mama na kupata kutoka katika bahari hii ya ilimu, kadri kile alichoweza kuchukua. Tangu mwanzoni, alipata utambuzi wa kisiasa hususan kutoka kwa zile harakati za kisiasa ambazo babu yake alizianzisha kuisaidia Khilafah ya Uthmaniyya. Sheikh huyu alinufaika pakubwa kutokana na majadiliano ya kifiqhi ambayo yaliandaliwa na babu yake Sheikh Yusuf. Ni wakati wa mijumuiko hii ndipo alipovutia umakinifu wa babu yake kwake. Hivyo basi, Sheikh Yusuf alimshawishi babake Sheikh Taqi kumpeleka Chuo Kikuu cha Al Azhar kwenda kupata ilimu ya ‘Uloom e Sharaii'.

Kupata ilimu:

Sheikh Taqi alipokewa na kujiunga katika daraja ya nane katika Chuo Kikuu cha Al Azhar mnamo 1928 na kumaliza mtihani wake kwa alama ya juu zaidi ya ‘Distinction’ mwaka huo huo. Alipewa cheti cha ‘Shuhada Al Ghurba’. Baada ya hapa alijiunga na kuliyya ya sayansi ambayo ilikuwa imeunganishwa na Chuo Kikuu cha Al Azhar wakati huo. Alikuwa akihudhuria makongamano ya kielimu ya wale wanavyuoni ambao babu yake alimuongoza kwao mfano ni Sheikh Mohammad Al Khizar Hussain (rahimahu Allah). Katika mbinu ya kizamani ya kusomesha iliruhusika kwa wanafunzi kuhudhuria halaqa za aina hiyo.  Sheikh an-Nabahani daima alibakia kuwa mwanafunzi hodari; hata ingawa pia alikuwa na majukumu ya kimasomo katika Kuliyya ya Sayansi, wakati huo huo pia alikuwa akihudhuria makongamano ya kielimu. Wanafunzi wenzake na walimu walikuwa wakimuonea wivu kutokana na kina cha ufahamu wake, alielimika kwa rai na mijadala ya kukinaisha, ambayo aliiwasilisha katika midahalo iliyofanywa jijini Cairo na biladi nyinginezo za Kiislamu.      

Sheikh alipata shahada hizi: Shahada ya Wastani kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar, Shahada tal Ghurba kutoka Al Azhar, kufuzu katika lugha ya Kiarabu na fasihi kutoka Cairo, Dar al' Uloom, shahada ya ukadhi kutoka Ma'had al ‘Aala – taasisi ya mafunzo ya mahakama iliyo unganishwa na Al Azhar na Shahada tal ‘Alamiah katika sharia kutoka Al Azhar (shahada ya uzamili) mnamo 1932 M.  

Afisi Alizofanya kazi Sheikh:

Sheikh alihudumu katika kitengo cha elimu ya sharia cha Wizara ya Al-Ma’arif hadi mnamo 1938 M. Kisha kupandishwa cheo na kupewa uhamisho katika Mahakama ya Sharia na kuteuliwa kuwa mwanasheria katika Mahakama Kuu ya Haifa. Baada ya hapo alipandishwa ngazi katika cheo cha Msaidizi wa Kadhi. Kisha alihudumu kama kadhi katika Mahakama ya Ramallah hadi mnamo 1948 M. Baada ya uvamizi wa Mayahudi kwa Palestina, aligura kwenda Syria lakini kisha kurudi Palestina mwaka huo huo na akateuliwa kuwa kadhi wa Mahakama ya Sharia ya Al-Quds. Kisha alihudumu kama kadhi wa Mahakama Kuu ya Sharia hadi mnamo 1950 M. Baada ya hapo, alijiuzulu wadhifa wa ukadhi na kuwa mwalimu katika Kuliyya ya ‘Uloom e Islamia ya Oman. Sheikh (rahimahu Allah) alikuwa bahari ya elimu; alikuwa gwiji katika kila fani ya ilimu. Alikuwa Mujtahid mkubwa na Muhadith.        

Vitabu vya Sheikh Taqi:

i. Nidhamu ya Uislamu

ii. Muundo wa Chama

iii. Fahamu ya Hizb ut Tahrir

iv. Nidhamu ya Kiuchumi katika Uislamu

v. Nidhamu ya Kijamii katika Uislamu

vi. Nidhamu ya Utawala katika Uislamu

vii. Katiba (Dola ya Khilafah)

viii. Utangulizi wa Katiba

ix. Dola ya Kiislamu

x. Shakhsiyya ya Kiislamu (Juzuu Tatu)

xi. Fahamu za Kisiasa za Hizb ut Tahrir

xii. Fikra za Kisiasa

xiii. Mwito wa Harara

xiv. Khilafah

xv. Tafakuri

xvi. Uwepo wa Akili

xvii. Nukta Kianzilishi

xviii. Kuingia katika Jamii

xix. Lislah al-Misr

xx. Al Ittifaqiyat as Saniya al Mastiya al Suriya wal Yamania

xxi. Hal Qadeeh Falasteen ‘ala Tareeqa tal Amreekya wal Engleezia

xxii. Nazrya al Faragh al Syasi Hol Mashroo’ Eezan Hawar

Na kuna mamia ya Makala ya kifikra, kisiasa na kiuchumi vile vile.

Baada ya kupigwa marufuku usambazaji wa vitabu na makala zake; natija yake ikawa ni kusambaza baadhi ya vitabu kwa majina ya wanachama wengine wa Hizb kama vile:

i.     Sera ya Kiuchumi ya Kuigwa

ii.    Upingaji wa Ujamaa wa Marx

iii.    Namna Khilafah Ilivyovunjwa    

iv.   Hukmu za Dalili katika Uislamu    

v.    Nidhamu ya Kuadhiwa ya Uislamu   

vi.   Hukmu za Salah    

vii.  Fikra ya Kiislamu     

Kabla ya kuasisi Hizb aliandika vitabu viwili: Anqaz Falasteen (Uokozi wa Palestina) na Risla tal ‘Arab (Barua kwa Waarabu).

Tabia na Sifa zake:

Zuhair Kahala, mwalimu ambaye alikuwa mkuu wa idara katika Chuo cha Sayansi alikuwa ni mwajiriwa katika chuo hicho katika kipindi hicho ambacho Sheikh Taqiuddin alianza kufanya kazi humo chuoni. Anasimulia, “Sheikh alikuwa mtu mwerevu, mwenye maadili mema na moyo safi. Alikuwa na shaksiyya yenye ikhlas, hadhi na nguvu. Uwepo wa umbile la Kiyahudi katika moyo wa ummah wa Waislamu lilimuhuzunisha napia kumkasirisha.”

Alikuwa na kimo cha wastani, alijengeka kiasi, mchapakazi mwerevu, mtu mwenye kujituma na mmakinifu katika mijadala. Alikuwa mbora katika kuwasilisha hoja zake. Hakuwa na msimamo wa kati na kati katika yale aliyo yaamini kuwa ni Haq, ndevu zake zilikuwa za wastani katika urefu na nywele za kijivu ndani yake. Utambulisho wake ulikuwa wakuvutia na mazungumzo yake yaliwavutia wengine. Hoja zake zilikuwa zikiwashangaza wengine. Hakupenda kushiriki mapambano yasiyokuwa na malengo, kushambulia watu kibinafsi na kwenda kinyume na maslahi ya Ummah. Alichukia kuona watu wanatekwa na maisha yao ya kibinafsi. Daima alikuwa na wasiwasi kuhusiana na hali ya Ummah. Alikuwa ni dhati ya msemo wa Mtume (saw) ambao maana yake ni: ((من لم يهتم بأمر المسلمين فليس منهم)) "Yeyote ambaye hajishughulishi na kusimamia mambo ya Waislamu sio mmoja wao." Alikuwa akiirudia hadithi hii tena na tena na kuwasilisha ushahidi wake. Alikuwa akielezea huzuni yake kuhusiana na Imam Ghazali (ra) muandishi wa kitabu cha Ahya al Uloom, kwa kujitia shughuli za kuandika vitabu katika zama ambapo kulikuwa na mashambulizi ya msalaba.

Kuanzishwa kwa Hizb ut Tahrir na Safari yake:

Sheikh Taqiuddin alichambua vyama, harakati na mashirika yale yaliyokuwepo kwa kina na kwa juhudi kubwa. Alifuatilia kwa makini mbinu, fikra, uingiliaji na kufeli kwao. Sheikh akazingatia kwamba kuwepo kwa Hizb kuwa ni muhimu kwa kusimamisha Khilafah na hivyo basi akavisoma vyama hivyo kwa msukumo huo. Baada ya kuvunjwa kwa Khilafah kwa kutumia mikono ya Mustafa Kamal Ataturk, Waislamu hawakuweza kusimamisha Khilafah licha ya kuwepo na harakati nyingi za Kiilamu. Uvamizi wa “Israel” mnamo 1948 katika ardhi ya Palestina na udhaifu wa Waarabu mbele ya umbile la Kiyahudi kwa ushirikiano na msaada wa Uingereza kupitia udhamini wa serikali za Jordan, Misri na Iraq zilithibitisha kuwa ndio chachu ya hisia za Sheikh Taqiuddin.  Hivyo basi, akaanza kuchambua sababu ambazo hatimaye zitapelekea katika mwamko wa Waislamu. Mwanzo, Sheikh alilenga kuamsha Ummah na kuandika vitabu viwili: Anqaz Falasteen (Uokozi wa Palestina) na Risla tal ‘Arab (Barua kwa Waarabu). Vitabu vyote viwili vilisambazwa mnamo 1950; vitabu hivi vilikuwa vya kifikra tu, ‘Aqeeda na ujumbe wa kweli wa Ummah ikimaanisha ujumbe wa Uislamu ukisema kwamba ni Uislamu pekee ndio msingi ambao Waarabu walitakiwa kutafuta mwamko. Ujumbe wa Waarabu wazalendo ulitofautiana pakubwa na ujumbe wa Sheikh. Ujumbe ambao ulikuwa unalinganiwa na Waarabu wazalendo ulileta pengo kubwa baina ya Ummah na ujumbe wa kweli wa Uislamu, ilhali wakiujadili kupitia fahamu za kimagharibi ambazo zilikuwa zinapinga ‘Aqeeda na misingi yake. Kisha Sheikh akazichunguza fahamu hizo ambazo ndizo zilizokuwa ndio nguvu ya msukumo wa Waarabu wazalendo na kuchambua mapendekezo yote yaliyowasilishwa kwake kuhusiana na hilo. Lakini hakukinaishwa na pendekezo hata moja.    

Kabla kuchukua uamuzi wowote, aliwasiliana na wanachuoni ambao alikuwa anawajua na wale aliokutana nao ndani ya Misri. Aliwasilisha kwa wanachuoni hao fikra ya kuanzisha chama cha kisiasa ili kuuamsha Ummah wa Waislamu na kuurudisha utukufu wake wa zamani. Kwa lengo hilo, alisafiri katika ardhi ya Palestina na kuwasilisha kwa wanachuoni na wanafikra maarufu fikra yake ambayo ilikuwa imekita akilini na moyoni mwake. Aliandaa semina kwa lengo hilo na kuwaita wanachuoni wakaribu na mbali ndani ya Palestina. Katika semina hii alijadiliana na wanachuoni kuhusu njia sahihi ya kuleta uamsho na kuwafikishia wahudhuriaji kwamba wanaelekea njia ya makosa na juhudi zao hazitozaa matunda. Wahudhuriaji wa semina hizo wengi walikuwa maafisa katika vyama vya Kiislamu, kisiasa na kizalendo. Pia aliweza kuwa na mazungumzo ya kina kuhusiana na masuala ya kisiasa tofauti tofauti ndani ya misikiti ya Al Aqsa, Al Khalil na maeneo mengine nyakati tofauti tofauti. Alikuwa akielezea hali halisi ya Arab League katika khutba hizo akisema wazi kwamba ni natija ya umagharibi ukoloni na kwamba ni moja ya zana za Wamagharibi, kwa msaada wake imeweza kudhibiti ardhi za Waislamu. Sheikh alikuwa akifichua njama za kisiasa za Wamagharibi na alikuwa akivunja pazia ya urongo wa mipango ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Alikuwa akiamsha hisia za kubeba majukumu miongoni mwa Waislamu na kuwalingania kuanzisha chama kisafi kwa msingi wa Uislamu.

Sheikh Taqiuddin alisimama kama mgombeaji katika uchaguzi wa Bunge la Wawakilishi; ambalo lilikuwa ni kamati ya ushauri tu. Lakini kutokana na maoni yake makali, uchangamfu wa kisiasa, mapambano ya kiuhakika yanayolenga kusimamisha chama kwa msingi wa Uislamu na kujifunga kiukamilifu kwa Uislamu,

Lakini hilo halikumvunja moyo Sheikh kutokana na uchangamfu wake wa kisiasa wala kudhoofisha uamuzi wake bali aliendelea na amali zake za mawasiliano na mijadala. Amali zake zilipelekea katika kufaulu kuwakinaisha wanachuoni, makadhi na wanafikra wa kisiasa maarufu katika kubuni chama cha kisiasa. Kisha akawasilisha kwa watu hawa maarufu ajenda na fikra ambazo zilikuja kuwa ndio turathi za thaqafa ya Hizb. Baadhi ya wanachuoni na wanafikra walikubali fikra zake na kuziridhia, hivyo basi amali zake za kisiasa za kuunda Hizb zikawa zimefika kileleni.  

Mji ulio na Baraka wa Al Quds ndio sehemu ambapo misingi ya Hizb iliweka; ndipo alipokuwa anafanyakazi katika Mahakama ya Upeo. Wakati huo, aliwasiliana na watu wengi maarufu kama vile Sheikh Ahmad Da'oor wa Qalqeela, Sayyadan Nimr wa Egypt, Daud Hamdan wa Ramallah, Sheikh Abdul Qadeem Zallum wa Al Khalil (Hebron), Adil al Nabulsi, Ghanim Abdu, Munir Shaqeer, Sheikh As'ad Bewiz Tamimi, n.k.

Mwanzoni, mikutano ilifanyika miongoni mwa waasisi na ilikuwa haina mpangilio maalum na ilifanyika kutegemea na hitajio. Aghalabu mikutano hii ilifanyika Al Quds au Al Khalil ambapo mada za kuwaalika watu wapya ili kujiunga na Hizb zilijadiliwa. Kituo cha mijadala kilikuwa ni katika mada muhimu za Kiislamu za kidharura kwa ajili ya utukufu wa Ummah. Hali hii iliendelea mpaka mwisho wa 1952 ambapo watu hawa waliamua kubuni chama cha kisiasa.

Mnamo Novemba 17, 1952 wanachama waasisi wa Hizb waliiomba Wizara ya Ndani ya Jordan ili kupewa kibali rasmi cha kuruhusiwa ili kubuni chama cha kisiasa. 

Wanachama hao walikuwa:

1. Taqiuddin an-Nabahani: Rais

2. Daud Hamdan: Makamu wa Rais na Katibu

3. Ghanim Abdu: Mweka hazina

4. Adil Al Nabulsi: Mwanachama

5. Munir Shaqeer: Mwanachama

Baada ya hapo, Hizb ikakamilisha matakwa yote ya kisharia yaliyohitajika kwa mujibu wa sharia ya Uthmaniyya kuhusiana na kuundwa kwa vyama. Makao makuu ya Hizb yalikuwa ni Al Quds na hatua zote zilizochukuliwa na chama hiki zilikuwa sahihi na kwa mujibu wa sharia ya Uthmaniyya.

Na kwa kuchapishwa kwa “Msingi wa Nidhamu ya Kiutawala na Masharti ya Kiidara” kutoka kwa Hizb katika Toleo Na.176 la gazeti la Al Sareeh lililotoka tarehe Machi 14, 1953; Hizb ut Tahrir ikawa chama cha kisharia kuanzia tarehe hiyo ikiwa ni sawa na Jamad ul Awal 28, 1372 Hijria. Hivyo basi, tokea siku hiyo Hizb ilikuwa imeidhinishwa na kuwa na haki ya kutekeleza amali za kisiasa kwa mujibu wa sharia ya Uthmaniyya ya wakati huo.  

Lakini, serikali ikawaita wanachama wote watano waasisi na kuwahoji na kuwakamata wanne miongoni mwao. Mnamo Rajab 7, 1372 Hijria sawia na Machi 23, 1953 kupitia taarifa, serikali ikapiga marufuku chama na kuwaagiza waasisi wake kusitisha amali zozote walizokuwa wanatekeleza. Mnamo Aprili 1, mabango yaliyokuwa yamebandikwa katika afisi zake ndani ya Al Quds yaliondoshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya serikali.

Lakini, Sheikh Taqi hakuyapa umuhimu marufuku hayo na kuendelea na kazi yake. Akiendelea kulingania ujumbe ambao Hizb ilikuwa imeasisiwa juu yake. Daud Hamdan na Nimr Misri walijitenga na majukumu ya uongozi mnamo 1956 na nafasi zao kuchukuliwa na Sheikh Abdul Qadeem Zallum na Sheikh Ahmad Da'oor. Wanachuoni hawa wakubwa kisha walikuwa viongozi wa Hizb na kutimiza majukumu yao juu ya ulinganizi huu wa baraka.    

Hizb ilianza kwa kuwapa watu thaqafa kwa pamoja katika maeneo ya mikusanyiko ya msikiti wa Al Aqsa ili kuleta uamsho wa maisha ya Kiislamu. Kutokana na amali zao bora, serikali ikaanza kubuni mbinu duni ili kuifanya Hizb kutojiunga na kuwa chama na mshikamano mkubwa. Kutokana na hali hizo Sheikh Taqi, akaondoka katika eneo hilo mwishoni mwa 1953 na mara mbili hakuruhusiwa kurudi. 

Sheikh Taqi aliondoka na kwenda Syria mnamo Novemba 1953, ambapo alikamatwa na serikali ya Syria na kupelekwa uhamishoni Lebanon, ilhali serikali ya Lebanon haikutaka kumruhusu kuingia nchini mwao. Lakini alipoomba ruhusa kutoka kwa mkuu wa polisi katika kituo cha polisi katika bonde la Al Hareer ili kumpigia simu rafiki yake, afisaa huyo akamruhusu. Sheikh Nabahani akampigia rafiki yake Mufti Sheikh Hassan Al ‘Ala na kumuelezea hali yake. Sheikh Al ‘Ala naye kwa haraka akawatishia maafisa wa Lebanon kwamba lau hawatomuachilia Sheikh Taqi kuingia nchini, ataeneza habari kwamba inayojiita serikali ya kidemokrasia haitaki kumruhusu mwanachuoni mkubwa kuingia katika nchi yao. Mamlaka za Lebanon zikahofia tishio hilo na kumruhusu Sheikh Taqi kuingia.

Sheikh Taqi alizama katika ulinganizi wa fikra zake baada ya kuingia Lebanon na hakukabiliwa na vikwazo vyovyote vikubwa katika kazi yake mpaka 1958. Ambapo serikali ya Lebanon ilihisi hatari kutokana na fikra zake wakaanza kumkazia Sheikh na hivyo basi, Sheikh kisiri akahamia Tripoli, Lebanon kutoka Beirut. Moja katika marafiki zake anaowaamini alituambia kwamba Sheikh aliwekeza muda mwingi katika amali za kusoma na kuandika. Alikuwa anafuatilia habari za dunia kupitia redio na kutoa taarifa bora za kisiasa. Alikuwa mchamungu kama jina lake lilivyomaanisha – Taqi: Mchamungu. Daima aliudhibiti ulimi wake na kutizama chini. Hakuwahi kusikika kuwa na matusi dhidi ya Muislamu yeyote, hakuwahi kusikika kumfedhehesha yeyote hususan wale madhaifu katika Uislamu aliotofautiana nao katika Ijtihad.

Ndani ya Iraq, Sheikh alikuwa makini mno kutafuta Nussrah. Kwa ajili ya lengo hilo, Sheikh mwenyewe alisafiri kwenda Iraq mara nyingi pamoja na Sheikh Abdul Qadeem Zallum ambaye alikuwa huko kwa ajili ya mawasiliano muhimu yanayojumuisha watu kama Abdul Salam Arif n.k. Miongoni mwa ziara hizo ilijumuisha safari ya mwisho ambayo alikamatwa ndani ya Iraq na kuteswa kinyama; kimwili na kiakili. Lakini waliomhoji walifeli kupata taarifa walizotamani kutoka kwa Sheikh. Alidumu katika kurudia maneno haya kwamba alikuwa ni mtu mzima ambaye lengo lake pekee lilikuwa ni kuzuru Iraq kwa ajili ya matibabu.  Hakika, Sheikh alikwenda huko kutafuata matibabu ya Ummah mgonjwa ikimaanisha Khilafah. Mamlaka za Iraq zilipokuwa zimeshindwa kupata habari zozote kutoka kwake, zilikata tamaa na zikamvunja mkono wake na kumfurusha nje ya nchi yake ilhali akiwa amejaa damu kutokana na mateso ya kidhalimu. Na alipokuwa amefurushwa Ujasusi wa Jordan uliujuza Ujasusi wa Iraq kwamba mfungwa huyo alikuwa ni Sheikh Taqi aliyekuwa anatafutwa kwa udi na uvumba na Ujasusi wa Iraq. Lakini, Alhamdulillah, muda haukuwa upande wao na Sheikh alikuwa amefika mbali kutoka pale walipokuwa wao.     

Sheikh Taqi alikuwa mvumilivu katika kujifunga kwake kubuni Hizb na alikuwa anakaribia kufikia sehemu aliyokuwa anaitamani, ndipo alipofariki.

Ummah huu mtukufu ulimuaga Sheikh Taqi mnamo Jumamosi, Fajr tarehe 02 Muharram 1398 Hijria sawia na 11 Disemba 1977 Miladi. Hakika alikuwa kiongozi mkubwa na bahari ya ilimu pasina shaka alikuwa ni mwanasheria wa zama hizi, muamshaji wa fikra ya Kiislamu, mwanafikra wa karne ya 20 na Mujtahid wa kweli na mwanachuoni wa kuigwa. Sheikh alizikwa katika maziara ya Al Ozaayi' ndani ya Beirut. Sheikh mwenyewe hakuweza kufurahia matunda ya juhudi alizozianzisha na kuwekeza maisha yake ndani yake. Hakuiona Dola ya Khilafah ambayo Hizb imeasisiwa kwa ajili yake. Lakini alimuachia amana ya jukumu hilo mrithi wake na mwandani wake mwanachuoni wa kuigwa Sheikh Abdul Qadeem Zallum na kukutana na Muumba wake.  Licha ya Sheikh kutoshuhudia kusimamishwa kwa dola kwa macho yake, lakini juhudi zake zilizaa matunda na Hizb imeenea katika kila sehemu ya dunia na fikra zake zimepokelewa na kukubaliwa na watu duniani kote. Mamilioni ya watu wametabban fikra zake na wale ambao wamesoma kutoka kwake wamefika katika kila pembe ya dunia. Mpaka hivi sasa, magereza ya wakandamizaji duniani yamejaa watu ambao wanaobeba na kulingania fikra zilizofanyiwa da’wah na Sheikh.  

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 16 Aprili 2020 06:24

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu