Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 7 Safar 1447 | Na: HTS 1447 / 12 |
M. Ijumaa, 01 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Yaandaa Kisimamo Mbele ya Msikiti Mkongwe jijini Port Sudan cha Kuinusuru Gaza
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan imeandaa kisimamo mbele ya Msikiti Mkongwe jijini Port Sudan leo, Ijumaa, 7 Safar 1447 H sawia na tarehe 1 Agosti 2025 M, baada ya swala ya Ijumaa. Wanachama wa Hizb waliinua mabango yenye alama ishara: “Angusheni viti vya utawala vinavyozuia kusonga kwa majeshi kuinusuru Gaza.” Mabango hayo yalisomeka:
- [وإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]
- Mpaka lini mutaendelea kuwafelisha watu wenu huko Gaza wakati mutaulizwa juu yao na Mwenyezi Mungu?!
- Lau tungekuwa na Khalifa, angetuamrisha (wasikivu na watiifu) kuswali swala ya Alasiri huko Palestina pekee.
- Enyi Ummah wa bilioni mbili: Je, ni rahisi kwenu kuwaona watu wa Gaza wakifa kwa mabomu ya mapipa, maroketi, na njaa huku mnatazama?
- Je, kuna uhalifu mkubwa zaidi kuliko kuweka majeshi kambini huku umbile la Kiyahudi likiwachinja wanawake, watoto na wazee wetu?!
- Enyi Umma wa bilioni mbili: Simamisheni Khilafah ili kuikomboa Gaza na ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.
- Umbile la Kiyahudi ni kivuli cha tawala zilizopo katika nchi za Kiislamu. Ikiwa kitu kitatoweka, kivuli chake hutoweka.
- Waislamu ni mkono mmoja dhidi ya wengine wote, basi munawezaje kuwasalimisha ndugu zenu wa Gaza kwa adui yenu?!
- Vipinduenu viti vichakavu vya utawala vya vibaraka na musimamishe Khilafah) ili iwanusuru ndugu zenu.
- Waumini ni ndugu, basi wanusuruni ndugu zenu mjini Gaza, ikiwa kweli nyinyi ni Waumini.
Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alihutubia waumini walipotoka msikitini. Waliingiliana na kisimamo hicho na hotuba hiyo kwa kupiga Takbira na Tahlil, wakionyesha mshikamano wao na kadhia ya Waislamu nchini Palestina, na wakasubiri hadi mwisho wa kisimamo hicho licha ya joto kali.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |