Ijumaa, 10 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sehemu Ambapo Hizb ut Tahrir Inafanya Kazi yake

Licha ya Uislamu kuwa ni mfumo wa kiulimwengu, lakini njia yake haimruhusu yeyote kuifanyiakazi kiulimwengu tokea mwanzoni. Lakini ni dharura kuilingania kiulimwengu na kuifanya sehemu ya kazi yake kuwa ni ndani ya nchi moja au nchi chache mpaka pale itakapoimarika hapo na dola ya Kiislamu itakaposimama.

Dunia yote ni sehemu mwanana kwa da'wah ya Kiislamu. Lakini kwa kuwa watu ndani ya nchi za Waislamu tayari wao wameukubali Uislamu, ni dharura kwamba da'wah ianze huko. Nchi za Kiarabu zinafaa zaidi kuwa sehemu ya kuanzia katika kubeba da'wah  kwa sababu nchi hizi zinajumuisha sehemu ya ulimwengu wa Waislamu ambao wakaazi wake ni watu wanaozungumza lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya Qur'an na hadith na ni sehemu muhimu ya Uislamu na msingi wa thaqafa yake ya Kiislamu.

Hizb ilianza kubeba da'wah ndani ya baadhi ya nchi za Waarabu. Kisha ikasonga na kupanua eneo lake la da'wah kimaumbile mpaka pale likaanza kufanyakazi katika nchi za Waarabu na nchi zisizokuwa za Waarabu kwa pamoja.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:54

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu