Amerika Yala Sanamu Lake Yenyewe!
- Imepeperushwa katika Amerika
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika Arabuni ya kabla ya Uislamu, baadhi ya Waarabu walikuwa wakitengeneza masanamu yao kutokana na tende; walipohisi njaa, wangekula miungu yao! Leo, historia inajirudia yenyewe, lakini kwa umbo gumu zaidi. Mfumo wa Kimagharibi ambao hapo awali uliinyanyua fahamu ya uhuru hadi kwenye hadhi takatifu—uhuru wa fikra, dhamiri, na dini; uhuru wa kuzungumza na kujieleza; uhuru wa kukongamana kwa amani; ushiriki wa kisiasa; ulinzi wa haki za walio wachache; na kukataza utesaji na kutendewa kikatili – sasa unasaliti maadili haya haya yanapokinzana na maslahi ya mabepari na kipote cha watawala.