Damu ya Mashahidi Haitalipishwa Kisasi isipokuwa kwa Kutokomeza Umbile la Kiyahudi
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Takwimu zilizochapishwa na Wizara ya Afya huko Gaza mnamo Alhamisi alasiri zilionyesha kuwa wengi wa wahasiriwa wa hujuma inayoendelea ya Mayahudi kwenye Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya Jumanne ni watoto, wanawake na wazee. Jumla ya mashahidi waliokufa kutokana na uchokozi huu imefikia 25, huku idadi ya waliojeruhiwa ikifikia 76.