Jumatano, 04 Shawwal 1446 | 2025/04/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  24 Ramadan 1446 Na: H 1446 / 100
M.  Jumatatu, 24 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umbile la Kiyahudi Linatekeleza Mauaji ya Halaiki na Unyanyasaji wa Kijinsia mjini Gaza. Je, Kuna Njia ya Kuamsha Uzembe Huu?
(Imetafsiriwa)

Tangu kutekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo 7 Oktoba 2023, umbile la Kiyahudi limewatenga watu walio na msimamo thabiti wa Gaza na kumwaga chuki yake juu yao. Limefanya mauaji ya mfululizo ambayo yamesababisha makumi ya maelfu kuuawa shahidi, huku Umma wa Kiislamu ukiwa bado umefungwa pingu na majeshi yake yamenyamaza kimya kama watu wa makaburini! Lilianza tena mauaji yake baada ya kukiuka usitishaji vita, kwa uungaji mkono wa wazi wa Magharibi na ushirikiano wa wazi na wa aibu wa tawala angamivu katika nchi za Waislamu.

Mnamo 13 Machi 2025, BBC ilichapisha makala kuhusu ripoti mpya iliyotolewa na Tume Huru ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, ambayo inanakili "ukiukwaji mkubwa" uliofanywa dhidi ya wanawake, wanaume na watoto wa Kipalestina tangu Oktoba 7, 2023. Ripoti hiyo ilijumuisha madai kwamba umbile la Kiyahudi lilifanya "vitendo vya mauaji ya halaiki kupitia uharibifu wa kimpangilio wa huduma za afya ya wanawake wakati wa vita dhidi ya Ukanda wa Gaza na matumizi ya unyanyasaji wa kijinsia kama mkakati wa vita."

Vitendo hivi ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya afya na vituo vya uzazi ili kuzuia uzazi, mauaji ya kina mama kwa kuzuia upatikanaji wa vifaa vya matibabu, na kuzuia huduma ya afya ya uzazi kwa kunyima dawa na vifaa muhimu ili kuhakikisha ujauzito, uzazi, matunzo baada ya kujifungua na huduma salama za watoto wachanga. Umoja wa Mataifa umeviainisha vitendo hivi kuwa ni vitendo vya mauaji ya halaiki na ukatili wa kijinsia. Hii ni pamoja na unyanyasaji wa kimaneno, kushambuliwa, vitisho vya ubakaji, na kulazimishwa kuwa uchi ili kuwadhalilisha zaidi wanawake.

Je, unyonge huu utaendelea hadi lini enyi Umma wa Waislamu bilioni mbili? Hadi lini Mayahudi wataendelea kufurukuta katika ardhi za Waislamu huku nyinyi mkikaa kimya kuhusu uhaini wa watawala wenu na kufeli kwa majeshi yenu? Je, kuna kitu chochote isipokuwa nguvu za majeshi yenu kinachoweza kulikomesha umbile la Kiyahudi?

Yeyote anayefikiri mfumo wa kimataifa utawasaidia watu wa Palestina amehadaika. Tumeona jinsi mfumo huo wa kihalifu ulivyowanusuru watu wa Bosnia na Iraq, pamoja na Waislamu wa Rohingya na Uyghur hapo awali!

Yeyote aliyetufanya tuamini kwamba Umoja wa Mataifa, ambao unalaani umbile la Kiyahudi kwa ripoti hizi za kuchukiza, utawatendea haki watu wa Palestina, basi aondoe pazia machoni mwake na azipitie ripoti zizo hizo ili aone kwamba zinadhamini kuwekwa wakfu kwa uwepo kwa umbile nyakuzi la Kiyahudi kama dola yenye haki ya kuwepo katika sehemu kubwa ya ardhi ya Palestina, na kuwaachia watu wa Palestina chini ya asilimia 20 ardhi hiyo ambayo wataasisi dola yao!

Enyi Waislamu, Enyi Majeshi ya Waislamu na Nchi Jirani hasa, yeyote miongoni mwenu anayedhania kuwa kimya chake kitazuia balaa hii isimfikie anajidanganya. Adui huyu hatutofautishi na anatuona sote kama walengwa kwenye orodha yake ya inayongojea. Mwenye kuamini kuwa ushindi (nasr) utakuja bila ya jihad, na kwamba izza itatoka kwa mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kwa mujibu wa sheria nyengine kinyume cha Shariah yake, amepata hasara duniani na Akhera, na hiyo ndiyo hasara iliyo wazi.

[يَدْعُو مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ * يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ لَبِئْسَ الْمَوْلَى وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ * إِنَّ اللهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ إِنَّ اللهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ * مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ اللهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى السَّمَاءِ ثُمَّ لْيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُ مَا يَغِيظُ]

“Badala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisicho mdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotolea mbali! Humuomba yule ambaye bila ya shaka dhara yake ipo karibu zaidi kuliko nafuu yake. Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu, na rafiki muovu. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kati yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo. Anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera na afunge kamba kwenye dari kisha aikate. Atazame je hila yake itaondoa hayo yaliyo mkasirisha?” [Al-Hajj 22:12-15]

Wanawake cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu