Ijumaa, 20 Shawwal 1446 | 2025/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Kampeni ya “Majeshi na Yaelekee Al-Aqsa”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa zaidi ya wanaume na wanawake 170,000 wa Kiislamu hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Pakistan inaandaa msururu wa amali kwa kichwa: “Majeshi na Yaelekee Al-Aqsa”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Gaza Inahitaji Majeshi Kuwapindua Watawala na Kutangaza Jihad”

Matembezi yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 13 Shawwal al-Khair 1446 H sawia na tarehe 11 Aprili 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath kunusuru watu wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa ulio mateka, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunisia chini ya kichwa: “Gaza Inahitaji Majeshi Kuwapindua Watawala na Kutangaza Jihad”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Matembezi Jijini Amsterdam “Harakati kwa ajili ya Gaza!”

Kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, Machi 18, 2025, na kuanza tena mauaji ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao ni wanawake, watoto, na wazee, Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa matembezi na kisimamo cha halaiki katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kwa kichwa: “Harakati kwa ajili ya Gaza!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Majeshi (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”

Matembezi yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 28 Machi 2025 sawia na tarehe 28 Ramadhan 1446 kuanzia Msikiti wa Al-Fath yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuinusuru Gaza dhidi ya uadui wa Marekani Mzayuni, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunis na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka Tunisia ya kijani. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likisomeka, “Enyi majeshi! (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?)”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Visimamo na Matembezi “Inatosha... Majeshi na yaelekee Al-Aqsa!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa msururu wa amali kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, 18 Machi 2025.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Dua ya Kunut “Kwa ajili ya Gaza... Mikono Imeinuliwa Mbinguni?!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa amali “Dua ya Kunut” kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, 18 Machi 2025, na kuanza tena mauaji yake ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao wakiwa ni wanawake, watoto na wazee, chini ya kichwa: Dua ya Kunut “Kwa ajili ya Gaza... Mikono Imeinuliwa Mbinguni?!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Amali za Usiku “Mutachukua Hatua Lini kwa ajili ya Gaza?!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa amali kubwa za usiku katika idadi kadhaa ya miji Uturuki kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne tarehe 18/03/2025.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu