Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Lengo la Hizb ut Tahrir

Lengo lake ni kurudisha tena mfumo kamili wa Kiislamu na kulingania da’wah ya Kiislamu Ulimwenguni. Lengo hili lamaanisha kuwaregesha Waislamu kuishi maisha kamili ya Kiislamu ndani ya Dar ul-Islam na ndani ya mujtama wa Kiislamu ambao kwamba mambo yote ya kimaisha yatasimamiwa kwa mujibu wa hukmu za kisheria, na kipimo ndani yake ni halali na haramu chini ya kivuli cha dola ya Kiislamu, ambayo ni dola ya Khilafah. Dola ambayo Waislamu watateua Khalifah na kumpa ahadi ya utiifu (Bay’ah) kumsikiza na kumtii kwa sharti kuwa ahukumu kuambatana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kwa sharti kuwa alinganie Uislamu kama risala ya kiulimwengu kupitia da’wah na Jihad.

Chama hiki, pamoja na hayo, kinalenga kufikia muamko sahihi wa Umma kupitia fikra angavu. Pia kinafanya bidii kuurudisha tena katika nguvu na izza yake ya mwanzoni kiasi ya kuuwezesha kunyakua uwezo wa kiathari kutoka kwa dola nyenginezo na kurudi mahali pake panapo stahili kama dola inayoongoza duniani, kama ulivyokuwa mwanzoni, ulipo utawala ulimwengu kuambatana na hukmu za Kiislamu.

Pia kinalenga kuurudisha uongofu wa Uislamu kwa wanadamu na kuuongoza Umma huu katika mvutano na ukafiri, nidhamu zake na fikra ili Uislamu utawale ulimwengu mzima.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:58

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu