Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Njia ya Hizb ut Tahrir

Njia iliyo tabanniwa na Hizb ut Tahrir kulingania da’wah ni njia ya kisheria iliyovuliwa kutoka katika seerah ya Mtume (saw) katika utendakazi wake katika ulinganizi wa da’wah. Hii ni kwa sababu ni wajibu kumfuata yeye, kama alivyosema Allah (swt):

Hakika nyinyi mnayo ruwaza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.”                 [Al-Ahzab: 21]

Sema: Ikiwa nyinyi mwampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutienii madhambi yenu.” [Aal Imran: 31]

Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.”              [Al-Hashr: 7]

Kuna aya nyengine nyingi zinazo ashiria uwajibu wa kumfuata Mtume (saw), kumfanya kiigizo na kuchukua mambo yote ya dini hii kutoka kwake.

Kwa kuwa Waislamu siku hizi wanaishi ndani ya Dar al-Kufr, kwa kuwa wanatawaliwa na sheria kinyume na zilizo teremshwa na Allah (swt), imezifanya ardhi zao kushabihiana na Makkah aliyotumilizwa Mtume (saw) kwa mara ya kwanza kama Mtume. Hivyo basi, ni muhimu kuichukua sehemu ya Makkah katika seerah ya Mtume (saw) kama mfano katika ulinganiaji da’wah.

Kwa kuisoma seerah ya Mtume (saw) mjini Makkah mpaka alipoweza kuasisi dola ya Kiislamu Madina, ni dhahiri kuwa yeye (saw) alipitia hatua za wazi, kila mojawapo yeye (saw) alikuwa akifanya matendo maalumu. Kwa hivyo chama hiki kimechukuwa kutokana nayo njia ya utendakazi wake, na hatua za matendo yake na amali zake ambazo ni sharti izitekeleze katika hatua hizi kuambatana na amali alizozifanya Mtume (saw) katika hatua hizi za kazi yake.

Kutokana na haya, chama hiki kimeifafanua njia yake katika hatua tatu:

Hatua ya Kwanza: Hatua ya kutoa thaqafa ili kuzalisha watu wanao amini fikra na njia ya chama hiki, ili waunde pote la chama.

Hatua ya Pili: Hatua ya maingiliano na Umma, ili kuufanya Umma ukumbatie na kuubeba Uislamu, ili Umma uuchukue kama kadhia yake, na hivyo basi kufanya kazi kuusimisha katika mambo yake ya kimaisha.

Hatua ya Tatu: Hatua ya kuasisi serikali, kutabikisha Uislamu kijumla na kiukamilifu, na kuubeba kama ujumbe kwa ulimwengu mzima.

Chama kilianza hatua ya kwanza katika eneo la al-Qudsi mnamo 1372 Hijri (1953 Miladi) chini ya uongozi wa muasisi wake, mwanachuoni muheshimika, mufakir, mwanasiasa shupavu, kadhi katika mahakama ya rufaa eneo la al-Qudsi, Taqiuddin al-Nabhani (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi). Katika hatua hii, chama kilikuwa kikiwasiliana na Umma kwa kuwasilisha kwao kupitia watu binafsi binafsi, fikra na njia yake. Kila aliye kubali fikra yake msingi, chama kilikuwa kikimuandalia masomo ya umakinifu katika duara (Halaqaat) zake za masomo, ili atakaswe kwa fikra na hukmu za Uislamu zilizo tabanniwa na chama na hivyo basi kujenga kwake utambulisho ‘shakhsiya’ wa Kiislamu. Hivyo basi anaingiliana na Uislamu na kuufurahia utambuzi (Aqliyya) wa Kiislamu na hamasa za Kiislamu zinazo mpelekea kuanza kubeba da’wah kwa watu. Pindi mtu anapofika hatua hii anajipendekeza kwa chama na hivyo basi kuwa mwanachama ndani yake. Hivi ndivyo alivyo fanya Mtume (saw) katika hatua yake ya kwanza ya da’wah, iliyoendelea kwa muda wa miaka mitatu, kwa kuwaita watu binafsi binafsi na kuwasilisha kwao yale aliyoteremshiwa na Allah (swt). Aliwakusanya kwa siri wale walio muamini katika msingi wa mfumo huu. Alikuwa na hamu ya kuwafunza Uislamu na kuwasomea yale yaliyo teremshwa na yaliyokuwa yakiteremshwa kwake mpaka akawayeyusha kwa Uislamu. Alikuwa akikutana nao kwa siri na kuwafunza sehemu zilizo fichika kutoka machoni mwa watu. Walikuwa pia wakifanya ibada zao kwa kujificha. Hatimaye, da’wah ya Uislamu ikaenea mjini Makkah, na watu wakaanza kuizungumzia na kuanza kuingia katika Uislamu kwa makundi.

Katika hatua hii ya da’wah, chama kikatuliza makini katika kujenga mwili wake, kuongeza uanachama wake na kutoa thaqafa kwa watu binafsi katika halaqaat zake kwa thaqafa makinifu ya chama mpaka kilipo faulu kuunda muundo wa chama kutokana na watu walio yeyushwa kwa Uislamu, na ambao wame tabanni fikra za chama na wakaingiliana na fikra hizi na kuzilingania kwa watu. Baada ya chama kufaulu kuunda muundo wake na mujtama kuanza kukijua na kukitambua pamoja na fikra zake na yale kinacho yalingania, chama kikaingia katika hatua ya pili.

Hatua hii ni ya maingiliano na Umma kuufanya ubebe Uislamu na kuasisi katika Umma utambuzi jumla na rai jumla juu ya fikra na hukmu za Uislamu zinazo tabanniwa na chama. Ili Umma uzitabanni kama fikra zake na kujitolea kuziasisi maishani, na kusonga mbele pamoja na chama katika kazi ya kuasisi dola ya Khilafah na kumteua Khalifah ili kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu na kubeba da’wah ya Uislamu ulimwenguni.

Katika hatua hii chama kilipanua mipaka ya matendo yake kutoka kuwa kinawafuata watu binafsi na kuwa kina zungumza na halaiki ya watu kwa ujumla. Katika hatua hii kilikuwa kikitekeleza kazi zifuatazo:

Utoaji thaqafa ya umakinifu kwa watu binafsi ndani ya halaqaat zake kujenga mwili wa chama na kuongeza uanachama wake, na kuzalisha utambulisho ‘shakhsiya’ wa Kiislamu ulio na uwezo wa kubeba da’wah na kusonga mbele katika mvutano wa kifikra na kisiasa. Utoaji thaqafa jumla kwa halaiki ya watu katika Umma kwa fikra na hukmu za Uislamu ambazo Hizb imezitabanni, kupitia madarasa, hotuba, na mazungumzo misikitini, vituoni na sehemu jumla zinazo kusanyika watu, na kupitia vyombo vya habari, vitabu na matoleo. Haya yalifanywa ili kuunda utambuzi jumla miongoni mwa Umma na kuingiliana nao.

Mvutano wa kifikra dhidi ya itikadi, nidhamu na fikra za kikafiri, fikra za kimakosa na fahamu ghushi kwa kufichua ubatili wake, dosari na kugongana kwake na Uislamu, ili kuutoa Umma kutokana nazo na athari zake.

Mvutano wa kisiasa, unawakilishwa kwa njia ifuatayo:

Mapambano dhidi ya dola kafiri za kikoloni zilizo zitawala na kuziathiri biladi za Kiislamu. Mapambano dhidi ya ukoloni katika sura zake zote; kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijeshi, ikihusisha kudhihirisha mipango yake, na kufichua njama zake ili kuutoa Umma kutokana na utawala wake na kuukomboa kutokana na natija yoyote ya athari yake.

Mvutano dhidi ya watawala katika biladi za kiarabu na za Kiislamu, kwa kuwafichua, kuwahisabu, kufanya kazi ya kuwabadilisha kila wanapo unyima Umma haki zake au kupuuza kutekeleza jukumu lao kwake, au kudharau lolote kati ya mambo yake, na kila wanapo kuwa kinyume na hukmu za Kiislamu, na pia kufanya kazi kuondoa tawala zao ili mahali pake kusimamisha utawala wa Kiislamu.

Kubeba maslahi ya Umma na kutabanni mambo yake kuambatana na hukmu za kisheria. Chama kimetekeleza kazi yote hii kwa kumuiga Mtume (swt) alivyo fanya baada ya Allah (swt) kumteremshia:

“Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirika.” [Al-Hijr: 94]

Mtume (saw) alitangaza ujumbe wake na kuwaita Maquraish katika mlima wa Safa na kuwaambia kuwa yeye ni Mtume aliye tumilizwa kwao. Aliwalingania kumuamini. Alianza kufanya ulinganizi wake kwa halaiki ya watu pamoja na watu binafsi binafsi. Maqureish walivyo mpinga, alipambana nao, miungu yao, itikadi zao na fikra zao, akifafanua upotovu, ufisadi na dosari zake. Alizidunisha na kuzishambulia kama vile pia alivyozishambulia itikadi na fikra nyenginezo zilizokuwako. Aliteremshiwa Aya za Qur’an mfululizo juu ya kadhia hizi na zilishutumu vitendo vya Maqureish vya ulaji riba, kuzika binti zao wakiwa hai, kupunja katika mizani na uzinifu. Aya pia ziliteremshwa kushambulia viongozi na machifu wa Kiqureish, zikiwahujumu wao, fikra zao na mababu zao, na kufichua njama zao dhidi ya Mtume (saw) na dhidi ya da’wah yake na Maswahaba zake.

Chama kilikuwa wazi, na kupambana katika ubebaji wake wa fikra zake na katika ukabilianaji wake na fikra na vyama vya kisiasa batili, katika mvutano wake dhidi ya makafiri wakoloni pamoja na mvutano wake dhidi ya watawala. Hakimpaki mafuta yeyote, wala hakimsifu yeyote, wala hakifanyi tahadhari au kuzingatia usalama, namna itakavyo kuwa matokeo au dhurufu za da’wah yake. kinapambana na kila anaye pinga Uislamu na sheria zake, jambo lililo pelekea kukabiliwa na madhara makubwa na yanayotekelezwa na watawala dhidi yake; kama vile kifungo gerezani, mateso, kutolewa nchi, kufuatiliwa, wanachama kuharibiwa kazi zao, kuharibu maslahi yao, kuwapiga marufuku ya kusafiri na mauaji. Watawala hawa dhalimu nchini Iraq, Syria, Libya na biladi nyenginezo wamewaua mamia ya wanachama wake. Magereza ya Jordan, Syria, Iraq, Misri, Libya, na Tunisia yamejaa wanachama wake. Chama kilipitia yote haya kupitia kufuata mfano wa Mtume (saw). Yeye (saw) ndiye aliyekuja na ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu mzima. Alipambana nao kwa hali ya wazi, na kuamini haki ambayo yeye (saw) alikuwa akiilingania. Yeye (saw) alipambana na ulimwengu mzima. Alivutana na kila aina ya watu pasi na ubaguzi, bila kutilia maanani mienendo yao, desturi zao, dini zao, itikadi zao, watawala au watu wa kawaida. Hakuzingatia hata kidogo jambo jengine lolote isipokuwa ujumbe wa Uislamu. Alichukua hatua dhidi ya Maqureish kwa kuiaibisha miungu yao. Alipambana nao juu ya itikadi zao na kuwahujumu akiwa yeye peke yake, pasi na kuwa na uwezo wa kutosha au wasaidizi na pasi na kuwa na silaha isipokuwa imani yake thabiti katika ujumbe wa Uislamu ambao yeye (saw) alitumilizwa nao. Ingawa chama kimejitolea kuwa wazi katika mapambano ya da’wah yake, kimejifunga katika vitendo vya kisiasa pekee na wala hakikuvuka na kutumia silaha dhidi ya watawala au dhidi ya wale wanaopinga da’wah yake, kwa kufuata mfano wa Mtume (saw) ambaye mjini Makkah alijifunga na ulinganizi pekee na yeye (saw) kamwe hakubeba silaha mpaka alipogura mjini Madina. Na pindi watu wa Bay’ah ya pili ya Aqabah walipopendekeza kwake kuwaruhusu kuinua upanga dhidi ya watu wa Mina, aliwajibu kwa kusema: “Bado hatujaamrishwa kwa hilo”. Na Allah (swt) akamwambia (saw) kuwa na subira juu ya mateso kwani Mitume kabla yake pia walipitia hayo, ambapo Allah (swt) aliwaambia:

Na hakika walikanushwa Mitume kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu.” [Al-An’aam: 34]

Kutotumia silaha kwa chama kujilinda au kukabiliana dhidi ya watawala haina uhusiano wowote na kadhia ya Jihad, kwa sababu Jihad ni yenye kuendelea mpaka siku ya Qiyama. Wakati wowote makafiri maadui watakapo shambulia biladi ya Kiislamu inakuwa ni wajib juu ya raia wake wa Kiislamu kumfurusha adui huyu. Wanachama wa Hizb ut Tahrir katika biladi hiyo ni sehemu ya Waislamu na itakuwa ni wajib juu yao kama ilivyo wajib juu ya Waislamu wengine, katika sifa yao kama Waislamu, kupigana na adui huyu na kumfurusha. Kunapo kuwa na Amir wa Waislamu aliyetangaza Jihad kuinua neno la Allah (swt) na kuwashajiisha watu kufanya hivyo, wanachama wa Hizb ut Tahri wataitikia mwito huo katika sifa yao kama Waislamu katika biladi hiyo ambayo mwito huo jumla wa kubeba silaha umetangazwa.

Pindi jamii ilipokosa kuitikia mwito wa chama kutokana na Umma kupoteza imani kwa viongozi wake na machifu wake ambao matarajio yake uliyaweka kwao. Dhurufu ngumu zilizo wekwa na eneo hili ili kurahisisha utekelezaji wa njama, dhulma na kukata tamaa ambako watawala wanatia dhidi ya watu wao na mateso makali wanayo tekeleza dhidi ya chama na wanachama wake, pindi jamii ilipokosa kuitikia mwito wa chama kutokana na sababu hizi chama kilianza kutafuta nusra kutoka kwa watu wenye msemo kikiwa na malengo mawili akilini mwake:

Kwa lengo la kupata hifadhi, ili kiweze kuendelea na da’wah yake huru na mateso. Kuchukua utawala ili kusimamisha Khilafah na kutabikisha Uislamu. Pamoja na kutekeleza vitendo vyote ilivyokuwa ikitekeleza, kama halaqaat za umakinifu, utoaji thaqafa jumla, ukilenga Umma na kuufanya ubebe Uislamu na kujenga rai jumla juu ya Uislamu kutokamana nacho. Kimeendelea kuvutana dhidi ya dola za kikafiri za kikoloni kwa kudhihirisha njama zao na kufichua khiyana zao, kama kinavyo endelea kuvutana dhidi ya watawala kwa kutabanni maslahi ya Umma na kuchunga mambo yao. Chama bado kinaendelea katika kazi yake na kutaraji kuwa Allah (swt) atakikabidhi kwake na kwa Ummah wa Kiislamu nusra, mafanikio na ushindi, na wakati huo Waumini watafurahia.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:49
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Tabbani ya Hizb ut Tahrir Fikra ya Hizb ut Tahrir »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu