Magereza ya Misri: Kati ya Mateso na Mauaji Pindi Heshima Inapokanyagwa Haki Huuawa!
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika tukio jengine la mara kwa mara la uhalifu uliofichwa, kijana mmoja aitwaye Ayman Sabry alikufa ndani ya kituo cha polisi katika Jimbo la Dakahlia kutokana na mateso ya kikatili, ambayo yaliacha alama wazi kwenye mwili wake. Chini ya masaa 48 baadaye, kijana mwengine alikufa ndani ya Kituo cha Polisi cha Al-Saff katika Jimbo la Giza, huku kukiwa na ripoti thabiti za kutelekezwa kimakusudi, dhulma, na ukatili, na kuvigeuza vituo vya polisi kuwa sehemu za vifo cha polepole.