Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uanachama wa Hizb ut Tahrir 

Chama kinawakubali Waislamu wanaume na wanawake kuwa wanachama wake pasina na kuzingatia kuwa ni Waarabu au la, au rangi fulani kwa kuwa ni chama cha Waislamu wote. Kinawalingania Waislamu wote kuubeba Uislamu na kutabban nidhamu zake pasina kuzingatia mataifa yao, rangi zao na madhhab zao kwa kuwatizama wote kwa mujibu wa mtizamo wa Uislamu.

Njia ya kuwaunganisha watu kwa Chama ni kupitia wao kuikubali 'aqeedah ya Kiislamu, kumakinika katika thaqafa ya Chama na kutabban fikra na maoni ya Chama. Mtu husika hujifunga kwa Chama, pale ambapo kitamyeyusha na wakati da'wah itaingiliana naye na kuzitabban fikra na fahamu za Chama. Kwa hiyo kiunganishi kinachowaunganisha wanachama wa Chama ni aqeedah ya Kiislamu na thaqafa ya Chama ambayo kiasili inatokamana na 'aqeedah hii. Halaqa za wanawake ndani ya Chama zimetenganishwa na halaqa za wanaume. Halaqa za wanawake zinasimamiwa ima na waume zao, jamaa zao ambao hawawezi kuwaoa au wanawake wengine.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:56
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Lengo la Hizb ut Tahrir Kazi ya Hizb ut Tahrir »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu