Matukio ya Uhalifu Yanayofichuliwa Katika Magereza ya Dhalimu wa Ash-Sham Yanapasa Kuwasha Moto Nyoyoni mwa Wana wa Ummah Kuwateketeza Watawala
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika siku chache zilizopita baada ya kutoroka kwa dhalimu Bashar na kuanguka kwa utawala wake muovu, matukio ya uchungu na makali yalifichuliwa ambayo yalivunja nyoyo za Waislamu. Kwani waliona kwa macho yao ukubwa wa jinai na ukatili ambao utawala wake uliamiliana nao kwa ndugu na dada zao katika vituo vya uzuizi na magereza: kuanzia na kuwekwa kwao kizuizini kwa miongo kadhaa katika magereza ambayo yalikosa mahitaji msingi zaidi ya kibinadamu, kisha njaa, ukandamizaji na mateso ya kikatili ambayo magereza hayo na kuta zinayazungumzia, na seli, nguzo na zana za mateso zinazosimulia hadithi zao, na miili ya wahasiriwa waliopatikana wamekufa na kukatwakatwa inamfichua.