Mkutano wa kilele wa Riyadh: Ushahidi kwa Usaliti wa Viongozi wa Waislamu dhidi ya Gaza na Lebanon
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Zaidi ya siku 400 baada ya vita vya mauaji ya halaiki vilivyoanzishwa na umbile nyakuzi, halifu la Kiyahudi dhidi ya watu wetu huko Gaza, vita ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia, na kufuatia mauaji na uharibifu uliofuata nchini Lebanon, viongozi wa Waislamu walikutana jijini Riyadh kwa kile walichokiita kuwa ni “mkutano wa ajabu.” Matokeo, hata hivyo, hayakuwa chochote ila mfululizo wa maamuzi dhaifu ambayo yanaweza tu kusifiwa kuwa ya khiyana.