Jumatatu, 23 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  7 Rabi' I 1447 Na: 1447 / 06
M.  Jumamosi, 30 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mateso ya watu wa Palestina kwenye Daraja la Mfalme Hussein (Allenby)
Kati ya Msongamano, Ufisadi, na Mfumo wa Hatari wa Tabaka la VIP

(Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia njama ya dola jirani  za eneo dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ili kukaza mzingiro dhidi ya watu wake, kuwadhuru, na kuwasukuma kuiacha ardhi yao na kuikabidhi kwa Mayahudi, Daraja la Mfalme Hussein (Allenby au Karameh) linaunda njia kuu ya maisha ya watu wa Palestina kwa ulimwengu wa nje. Hata hivyo, kivuko hiki, ambacho kinapaswa kuwa njia ya usafiri, kimekuwa chanzo cha mateso ya kila siku kwa wasafiri, hasa upande wa Jordan, ambapo mambo ya kibinadamu, ya kiutawala, na ya kisiasa yanaingiliana na kuunda mandhari katili sana.

Safari ya kuvuka katika pande zote mbili kupitia daraja hilo inaweza kuchukua masaa mingi, wakati mwingine kuzidi masaa kumi, katika hali ambazo zinakosa kiwango cha chini cha huduma za kibinadamu. Wazee, wagonjwa, na wanawake wanateseka maradufu, kwa kuwa hakuna viti vya kutosha wala mahali palipotayarishwa kwa ajili ya kusubiri kwa utulivu, huku joto kali katika msimu wa kiangazi na baridi kali katika msimu wa baridi zikiongeza uzito kwa wanayoyapitia wavukaji.

Kilichofanya mambo kuwa mabaya zaidi ni kwamba mamlaka za Jordan hivi karibuni zilianzisha mfumo wa ulipiaji tiketi wa mapema kupitia afisi maalum za usafiri, kwa kisingizio cha kupunguza msongamano na kupangilia trafiki. Hata hivyo, ukweli ulionyesha kwamba mfumo huu uligeuka kuwa njia ya ukiritimba, rushwa, na kizuizi kwa wasafiri; kwa kuwa ilikuwa vigumu kwa msafiri wa kawaida kupata nafasi ya karibu, kufungua mlango kwa ajili ya soko jeusi na madalali wa tiketi, ambao mara nyingi ni watu wa serikali, hasa wale wanaofanya kazi kwenye daraja lenyewe. Wasafiri wanalalamika kuwa madalali wanaoshirikiana na baadhi ya afisi hununua tiketi hizo na kuziuza kwa bei maradufu. Kitendo hiki kimekuwa mzigo wa ziada kwa familia za Wapalestina ambao wanalazimika kulipa kiasi kikubwa ili kupata hifadhi ya haraka, kufichua njama iliyopangwa na kufungua mlango wa ufisadi na unyang'anyi, pamoja na ushirikiano wa serikali ya Jordan na umbile la Kiyahudi katika mchakato wa kuwabana watu wa Palestina kuwahamisha kwa nguvu hadi kwenye ardhi na kuwafanya kukimbia mateso ya kusafiri kuingia au kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa.

Pamoja na soko jeusi, mfumo wa VIP unaimarisha aina ya wazi ya ubaguzi; kwa malipo ya kiasi kikubwa, kinachozidi dinari 150 za Jordan kwa kila mtu, wasafiri hupokea matibabu maalum ambayo yanajumuisha kupita foleni, kufupisha taratibu, na kusafiri kwa mabasi yenye viyoyozi. Huduma hii imegeuza kivuko hicho kuwa mandhari iliyoegemezwa juu ya tabaka; yeyote mwenye pesa hupita upesi, na asiye na pesa hubakia mateka kwenye foleni ndefu. Wanaofaidika na huduma hii wengi wao ni watu wa serikali ya Jordan wanaoshirikiana na Mayahudi katika kuwanyonya watu, kuwapora mali zao, na kuzigawanya baina yao.

Jambo hilo halikomei kwenye msongamano na ufisadi, bali linaenea hadi katika mwelekeo wa kina wa kisaikolojia na kisiasa; mateso kwenye daraja yanaonekana na Wapalestina kama udhalilishaji wa kiserikali, na kama ujumbe usio wa moja kwa moja kwamba matembezi yao hayako huru, na kwamba kusafiri kwao kunategemea uwezo wao wa kifedha au uvumilivu wao kwa mateso ya muda mrefu. Badala ya kuwa daraja la uunganishaji, limekuwa nembo ya kupoteza heshima na tofauti ya kijamii.

Na msafiri anachanganyikiwa ni nani kati ya pande hizi mwenye nia chafu zaidi: Mamlaka ya Palestina, umbile la Kiyahudi, au Jordan? Kwani kila mmoja wao humimina ghadhabu yake juu ya msafiri. Upande wa Mamlaka ya Palestina unafanana na kituo cha ukaguzi wa forodha, ambapo wanapekua watu na kuwanyang'anya bidhaa zao za kibinafsi kwa kisingizio kwamba wao ni ukiritimba wa kipekee wa Abbas, mwanawe Tareq, na wengine katika “wachezaji wakuu” wa Mamlaka ya Palestina. Ama upande wa Mayahudi, unafanya ukaguzi wa usalama kwa watu na mizigo, unawatoza ada kubwa watu wa Palestina kuondoka, kuwanyang'anya pesa zao, na kuwawajibisha kulipa faini na kodi kwa bidhaa zao za kibinafsi. Upande wa Jordan, hutoza ushuru wa kuingia Jordan na ushuru wa kutoka uwanja wa ndege, na kuwabana wasafiri kwa mfumo wa kukata tiketi mapema, na kuwasukuma kutumia huduma za VIP ambazo wengi hawawezi kuzimudu, haswa kwa vile hazizidi kuwasafirisha kwa umbali usiozidi kilomita tatu, kwa malipo ya gharama ambayo inaweza kuzidi dinari 150 kwa kila mtu.

Mmoja wa wasafiri alitoa mukhtasari wa kuteseka kwake baada ya kumaliza taratibu hizo upande wa umbile la Kiyahudi akisema: “Unatoka upande wa serikali ya Kiyahudi ambako unatendewa unyama, ila tu kuingia upande wa Jordan kana kwamba unaingia kuzimu ndogo ya mateso.” Daraja hilo limekuwa kielelezo tosha cha jinsi haki ya kutembea inavyoweza kugeuzwa kuwa mzigo wa kiuchumi na kisaikolojia, ambapo njama dhidi ya uthabiti wa watu wa Palestina katika ardhi yao iliyobarikiwa inaingiliana na ufisadi, ukiritimba, na utabaka.

Kwa hakika, yeyote anayetazama hali ya daraja hilo anatambua mukhtasari wa njama iliyosukwa na Mayahudi, pamoja na zana za utekelezaji; Mamlaka ya Palestina na utawala wa Jordan kwa lengo la kuwabana watu wa Palestina, kudhoofisha azma na uthabiti wao, hadi wakaamua kuikimbia Ardhi hiyo Iliyobarikiwa ili kuiacha wazi kwa Mayahudi. Serikali ya Jordan inasalia kuwa mlinzi mtiifu kwao kwenye mpaka mrefu zaidi, huku Mamlaka ya Palestina ikiendelea kufanya kazi kama jasusi na chombo cha usalama kwa Mayahudi kwa yeyote anayebakia katika watu wa Palestina. Lakini sio mbali, sio mbali, kwa Ruwaibidha (watawala watepetevu na duni), pamoja na maadui wa Mwenyezi Mungu, Mayahudi, kubadilisha hukmu ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake. Mtume (saw) amesema: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ فَيَقْتُلَهُمُ الْمُسْلِمُونَ، حَتَّى يَخْتَبِئَ الْيَهُودِيُّ وَرَاءَ الْحَجَرِ أَوِ الشَّجَرِ، فَيَقُولُ الْحَجَرُ أَوِ الشَّجَرُ: يَا مُسْلِمُ يَا عَبْدَ اللَّهِ، هَذَا يَهُودِيٌّ خَلْفِي، فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ، إِلَّا الْغَرْقَدَ فَإِنَّهُ مِنْ شَجَرِ الْيَهُودِ»  “Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na watawaua mpaka Mayahudi atajificha nyuma ya mawe au miti nao utasema: Ewe Muislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa Myahudi nyuma yangu basi njoo umuuwe. Isipokuwa mti wa Gharqad, kwani ni huo mti wa Mayahudi.” [Musnad Ahmad]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu