Jumatatu, 21 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni Dhambi Kubwa kwamba Gaza Haikukombolewa Au Umbile la Kiyahudi Halikutokomezwa kwa Juhudi za Wanajeshi wa Waislamu, Bali Iliangamizwa Kabisa na Kukombolewa Kidogo kwa Mpango Wa Trump na Usaliti wa Watawala wa Waislamu!!
(Imetafsiriwa)

Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]

Lakini kwa nini wanasherehekea na kumpongeza Trump, wakati yeye ndiye muungaji mkono mkuu wa umbile la Kiyahudi katika kuangamiza nyumba, miti na mawe ya Gaza!?

Kwa nini wanasherehekea wakati nukta ya tisa ya mpango huo inaeleza kuwa Gaza “itatawaliwa chini ya utawala wa mpito wa muda wa kamati ya wajuzi, ya kisiasa ya Palestina, yenye jukumu la kutoa huduma za kila siku za umma na manispaa kwa watu wa Gaza. Kamati hii itaundwa na wataalamu waliohitimu wa Kipalestina na wa kimataifa, huku uangalizi na usimamizi wake ukifanywa na bodi mpya ya mpito ya kimataifa “Bodi ya Amani,” ambayo itaongozwa na uenyekiti wa Rais Donald J. Trump, huku wanachama wengine na marais wa nchi wakitangazwa, akiwemo Waziri Mkuu wa Zamani Tony Blair.”?!!

Kwa nini wanasherehekea wakati nukta ya kumi na tatu ya mpango huo inasema, “Miundombinu yote ya kijeshi, ya kigaidi, na ya mashambulizi, ikiwemo mahandaki na vituo vya uzalishaji wa silaha, vitaharibiwa na havitajengwa upya. Kutakuwa na mchakato wa kuondolewa nguvu za kijeshi kwa Gaza chini ya usimamizi wa wachunguzi huru, ambayo itajumuisha uwekaji nje wa kudumu wa silaha, kupitia mchakato uliokubaliwa wa upokonyaji silaha unaoungwa mkono na mradi wa kimataifa wa ununuzi wa silaha hizo na uoanishaji upya, ambayo yote yatathibitishwa na wachunguzi huru…”?!

Na kwa nini wanasherehekea wakati jeshi la umbile la Kiyahudi litasalia katika udhibiti wa karibu 53% ya eneo la Ukanda wa Gaza [na baada ya kukamilika kwa uondokaji, jeshi la Israel litaendelea kuwa na udhibiti wa zaidi ya nusu ya eneo la Ukanda wa Gaza, kwa kiwango cha karibu asilimia 53 ... Maeneo haya: maeneo ya usalama katika mpaka wa Gaza, ikiwemo ukanda wa Philadelphi “mpaka kati ya Misri na Gaza), ikiongezewa na Beit Hanoun na Beit Lahia katika kaskazini ya mbali ya Ukanda huo, milima kwenye viunga vya mashariki mwa Mji wa Gaza, na sehemu kubwa za Rafah na Khan Yunis kusini mwa Ukanda huo...” (Asharq Al-Awsat, 10/10/2025)]?!

Kwa nini wanasherehekea wakati uondokaji utakuwa hadi Mstari wa Majano, ambao uko ndani ya Ukanda wa Gaza? “Mstari wa Manjano ni mstari wa uondokaji iliotengwa kwa ajili ya jeshi la Israel chini ya makubaliano. Ingawa Mstari wa Manjano uko kilomita kadhaa kutoka mpaka wa dola hiyo vamizi na Ukanda wa Gaza, maeneo mengi ya jeshi la Israel kwa sasa yapo kilomita moja na nusu kutoka mpaka huo...” (Al-Araby Al-Jadeed, 11/10/2025)?!!

Kwa nini wanasherehekea wakati watu wa Gaza wanahama kutoka sehemu moja hadi nyengine, wakiwa wamepoteza mashahidi wao: wanaume, wanawake, na watoto; na wakifika majumbani mwao wanazikuta zimeharibiwa, zikiwa sio makao hata kwa mkaazi wala mkimbizi?!

Kwa nini wanasherehekea, wakati kuna kituo cha uratibu wa kijeshi na kiraia kwa Ukanda wa Gaza kinachoongozwa na Kamandi Kuu ya Marekani? [CNN ilimnukuu afisa mmoja wa Marekani jana, Ijumaa, akisema kwamba vikosi vya Marekani vimeanza kuwasili nchini “Israel” ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuanzisha kituo cha uratibu wa kijeshi cha kiraia kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano... Mtandao wa Marekani umemnukuu afisa huyo akisema kuwa vikosi hivyo vitafuatilia “juhudi za kufikia utawala wa kiraia katika Ukanda wa Gaza” (Asharq Al-Awsat, 11/10/2025]?!

Je, hii ndiyo sababu wanasherehekea? Na wanakimbilia kumwalika Trump aongoze sherehe hiyo na kumpigia makofi, wakieleza kuwa ni tukio kubwa la kihistoria?! Ijapokuwa mpango wake ni kuwatia nguvu Mayahudi na kupoteza ardhi za Waislamu, ardhi iliyobarikiwa ya Palestina!! Je, hivi ndivyo watawala wa Waislamu wanavyomchukulia Trump na wakoloni makafiri kuwa washirika wao?

[تَرَى كَثِيراً مِنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ أَنْ سَخِطَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ]

“Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na walio kufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu.” [Al-Ma’idah: 80]

Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu: Makruseda, waliokusanyika kutoka Ulaya, walishambulia ardhi za Waislamu na wakabakia Al-Quds kwa miaka mingi, wakifanya uharibifu. Mapigano yaliendelea mpaka wanajeshi wa Uislamu, wakiongozwa na Salahudin, wakapigana nao na kuwashinda katika kushindwa kulikostahiki. Kisha Salahudin akaukomboa mji huo na kuwatoa humo, kwa kuwaua na kuwadhalilisha. Watu wake wakaregea humo wakiwa wameshinda na kutukuzwa.

Je, hamuna uwezo, enyi askari wa majeshi ya Waislamu, wa kufuata mfano wa wale waliokutangulieni miongoni mwa askari wa Uislamu kuikomboa Palestina na Ukanda wa Gaza Hashim kwa kulisaga saga umbile la Kiyahudi na kulitokomeza kabisa kutoka uwepo, ili watu wa Gaza, na kwa hakika Wapalestina wote, waweze kuregea majumbani mwao, wakiwa na heshima na ushindi, wakiongozwa takbira za ushindi, “Allahu Akbar”?

Hakika, munao uwezo! Kwani munalizunguka umbile la Kiyahudi kama bangili inavyozunguka mkono. Walakini, munahitaji kiongozi mwenye ikhlasi na mwaminifu. Je, hakuna kiongozi wa namna hii miongoni mwenu wa kukuongozeni katika vita dhidi ya adui yenu, ambaye amepatwa na unyonge na taabu, na ambaye hawezi kushinda katika vita dhidi yenu?

[وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [Aal-i-Imran: 111] Kisha mupigane nao katika vita vitakavyowatawanya walio nyuma yao, na kundi lao litashindwa na wao watakimbia.

Hakika, munao uwezo! Basi mtegemee Mola wenu Mlezi, na muimarishe azma yenu, na muwe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewasifu wakiwa wanapigana na adui yao, akisema:

[قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَنْ يُصِيبَكُمُ اللَّهُ بِعَذَابٍ مِنْ عِنْدِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُمْ مُتَرَبِّصُونَ]

Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” [At-Tawbah: 52].

Endapo watawala watakuzuieni kupigana na adui yenu, basi wapigeni vita kwa njia zote na mumnusuru Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni. Kisha watu wa Gaza, na kwa hakika Palestina yote, watarejea majumbani mwao wakiwa washindi, wakimtukuza Mwenyezi Mungu, na wakimshinda adui yao, wakiangamiza umbile lake. Badala ya kurudi kuona adui yao akitawala Ardhi Iliyobarikiwa kwa usaidizi wa Trump na kufeli kwa watawala Ruwaybidha (wajinga wasio na maana)!!

Enyi Waislamu... Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu:

Tunahitimisha kwa kile tulichokwambieni zaidi ya mara moja:

Tumehakikishiwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, izza ya Uislamu na Waislamu, kuregea kwa Khilafah Rashida, yenye kupigana, kuwapiga vita na kuwauwa Mayahudi, na kutekwa kwa Roma kama ilivyotekwa Konstantinopoli, na Istanbul ikawa nyumba ya Uislamu... Tumehakikishiwa hilo, hata kama makafiri na wanafiki watasema (kama ilivyo katika aya):

[إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَإِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima. [Al-Anfal: 49]. Hakika, ushindi wote huu kwa Waislamu ni katika ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw), na itatokea Mwenyezi Mungu akipenda... Lakini njia ambayo Mwenyezi Mungu, Al-Aziz Al-Hakeem (Mwenye nguvu, Mwenye hekima), anaitaka sio ateremshe Malaika kutoka mbinguni ili kutusimamishia Khilafah kwa ajili yetu na kutimiza kwa ajili yetu Ahadi ya Mwenyezi Mungu Al-Qawii Al-Aziz, na bishara njema ya Mtume Wake (saw) huku tukiwa tumekaa tuli bila kufanya chochote. Bali anateremsha Malaika kutusaidia na hali tunafanya kazi kwa umakini, bidii, ukweli, na ikhlasi... Kisha Mwenyezi Mungu ataturuzuku ushindi na kufuzu katika maskani zote mbili, na huko ndiko kufuzu kukubwa.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [Ar-Rum: 4-5]

Kwa hili, Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakulinganieni. Inakulinganieni enyi askari katika majeshi ya Waislamu. Kimbilieni utukufu wa duniani na Akhera. Songeni kulingamiza umbile la Kiyahudi na kurudisha Ardhi iliyobarikiwa yote kwenye nyumba ya Uislamu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi wala hatazipoteza amali zenu.

H. 20 Rabi' II 1447
M. : Jumapili, 12 Oktoba 2025

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu