Ijumaa, 14 Safar 1447 | 2025/08/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kitengo cha Wanawake “Kampeni ya Kimataifa - Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua kampeni ya kimataifa kuangazia maafa yanayozidi kuwa mabaya ya kibinadamu yanayowakabili Waislamu wa Sudan. Kampeni hii pia itashughulikia: siasa na ajenda zilizofichwa nyuma ya mzozo huu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Matembezi ya Halaiki ya Kuinusuru Gaza “Kuwahutubia wale Wanaohusika!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 21, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 200,000 Waislamu hadi sasa. Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa matembezi makubwa ya halaiki kote nchini Uturuki licha ya serikali ya Uturuki kuyapiga marufuku.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Matukio Mjini Al-Suwayda

Axios iliripoti kwamba mkutano wa ngazi ya juu ulifanyika jijini Paris kati ya Waziri wa Mambo ya Kimikakati wa ‘Israel’ Ron Dermer na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad Al-Shibani, uliopatanishwa na mjumbe maalum wa Marekani nchini Syria, Thomas Barak, mnamo 25/7/2025. Siku chache zilizopita tangu tarehe 12/7/2025 zimeshuhudia kuongezeka kwa machafuko katika Jimbo la Al-Suwayda [Sweida] kusini mwa Syria, ambalo wengi wa wakaazi wake ni Druze. Umbile la Kiyahudi limetangaza kuingilia kati masuala yao sambamba na kuendeleza uvamizi na mashambulizi yake nchini Syria. Lilishambulia pambizoni mwa kasri la rais, na kuishambulia Wizara ya Ulinzi na Majeshi jijini Damascus.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu