Matukio ya Umwagaji damu huko Sweida Yafichua Hatari za Makundi Yenye Uhusiano wa Kigeni Uhalalishaji Mahusiano ni Jinai Inayohujumu Miaka 14 ya Muhanga wa Mapinduzi
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kufuatia siku kadhaa za mapigano makali yaliyogharimu maisha ya mamia ya ndugu zetu waliokufa shahidi, Wizara ya Ulinzi ghafla na kwa mshtuko ilitangaza Jumatano kuwa ni siku ya kuanza kujiondoa kwa jeshi la Syria katika mji wa Sweida. Haya yanajiri baada ya wito wa Marekani wa kuondoa vikosi vya serikali katika jimbo hilo na msururu wa mashambulizi makali ya anga yaliyofanywa na umbile la Kiyahudi mjini Damascus siku ya Jumatano, Julai 16, 2025, yakilenga jengo la Jeshi, Wizara ya Ulinzi na maeneo jirani ya Kasri la Rais. Mashambulizi ya awali yalikuwa yamepiga maeneo mengi viungani mwa Damascus, Daraa na Sweida, yakilenga maeneo ya kijeshi na misafara ya jeshi la Syria na vikosi jumla vya usalama vilivyokuwa vikielekea Sweida, na kusababisha idadi kubwa ya mashahidi na majeruhi.