Afisi ya Habari
Wilayah Syria
H. 13 Ramadan 1446 | Na: 14 / 1446 H |
M. Alhamisi, 13 Machi 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Aqida ya Kiislamu Pekee ndiyo Msingi wa Dola, Katiba, na Sheria
Lengo ni Uislamu Uingie Madarakani na sio Kutosheka na Muislamu Kuingia Madarakani
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe mbili ya mwezi huu, Afisi ya Rais wa Syria kwa Kipindi cha Mpito ilitangaza kuundwa kwa kamati ya wataalamu ili kuandaa tangazo la katiba la kudhibiti kipindi cha mpito nchini Syria. Kamati hiyo itaiwasilisha leo, Alhamisi,13/3/2025, kwa Rais wa Syria kwa Kipindi cha Mpito, Ahmed al-Sharaa, aliyeiidhinisha. Kamati hiyo ilithibitisha kwamba tangazo hilo linadumisha jina la nchi kama “Jamhuri ya Kiarabu ya Syria,” linabainisha dini ya mkuu wa nchi kama “Uislamu,” linadumisha fiqhi ya Kiislamu kama chimbuko msingi la sheria, na linahakikisha mgawanyiko kamili wa mamlaka. Pia linaelekeza kuvunjwa kwa Mahakama ya Katiba iliyopo, kuanzishwa kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano, kuundwa kwa kamati ya kutunga katiba ya kudumu, na Bunge la Wananchi litachukua mamlaka ya kutunga sheria, huku Rais wa Jamhuri atachukua mamlaka ya utendaji.
Uislamu umetuwajibisha kuifanya Aqiyah (itikadi) ya Kiislamu kuwa msingi wa dola, na wakati huo huo, msingi wa katiba na sheria. Yaani, chanzo pekee cha sheria. Haupaswi kuambatanishwa na vyanzo vyengine vya sheria, kama ilivyo katika katiba zilizotungwa na mwanadamu; baadhi yazo zinadai kwamba Uislamu ndio chanzo kikuu au chanzo msingi cha sheria, huku kiuhalisia wanaazima sheria ngeni kwetu kutoka Magharibi.
Watu wa Ash-Sham: Ili serikali na dola ziwe za Kiislamu, itikadi ya Kiislamu lazima iwe chanzo pekee cha sheria. Hapo ndipo tunaweza kusema kuwa katiba ni ya Kiislamu. Kitu chengine chochote isipokuwa hicho ni kufuata tu mfano wa dola zengine na sheria ambayo zimetuwekea. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلا يَضِلُّ وَلا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا]
“…basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [TA-HA: 123-124]. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 40].
Enyi Waislamu wa Ash-Sham, Ash-Sham yenye Fahari, Ushujaa, na Uislamu: Ni hukmu na dola ya Uislamu pekee ndiyo itakayoinua hadhi yenu, kulinda heshima yenu, na kuwashinda maadui zenu. Kupitia subira yenu, uthabiti, na kujitolea mhanga kwa muda wa miaka 13, mumethibitisha kwamba kweli nyinyi ni vizazi vya masahaba na washindi walioinywesha ardhi ya Ash-Sham kwa damu yao ili dini hii tukufu ikufikieni. Kwa tamko lenu zuri sana: “Kiongozi wetu milele ni bwana wetu Muhammad,” mumethibitisha kwamba hamtakubali badali yoyote ya utawala wa Uislamu, kwani hilo pekee linatosha kuilipa ujira damu yenu iliyomwagika na kafara zenu zilizotolewa. Basi simameni imara katika jambo mlilotoka kwa ajili yake, ili Uislamu peke yake utekelezwe chini ya dola ambayo mfumo wake wa utawala ni Khilafah ambao Mtume wetu (saw) ametupa bishara njema ya kuregea kwake kwa kauli yake: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”. Dola ambayo itakuwa ni Usimamizi jumla kwa Waislamu wote, kuunganisha makundi yao yaliyotawanyika, kuunganisha nguvu zao, na kuregesha Al-Quds yao na Msikiti wa al-Aqsa kutokana na unajisi wa Mayahudi. Dola ambayo haitambui mipaka ya kitaifa au kikanda iliyochorwa na wakoloni makafiri kwa mikono yao miovu.
Enyi Watu wa Ash-Sham: Jueni kwamba hairuhusiwi kuwa na mfumo wa serikali wa jamhuri, ambao ndani yake sheria ni za wanadamu badala ya Mwenyezi Mungu. Pia hairuhusiwi kuwa na ufalme, himaya, au kitu chengine chochote. Waislamu hawatakuwa na usalama, hadhi, na maisha ya starehe isipokuwa kwa mfumo wa utawala unaomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw).
Enyi Watu wa Kujitolea, Enyi Ambao Mwenyezi Mungu Amewapa Ushindi na Heshima: Ni wakati sasa wa sisi kumridhisha Mwenyezi Mungu bila ya kuogopa chochote kutoka mashariki au magharibi, kwani Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki zaidi hofu yetu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[أَتَخْشَوْنَهُمْ فَاللهُ أَحَقُّ أَنْ تَخْشَوْهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]
“Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [At-Tawbah: 13].
Ndiyo, umefika wakati sasa wa sisi kujitahidi kukomesha zama za utawala wa kidhalimu ambao umeupigisha magoti Ummah wetu na kutuangamiza. Hamu yetu kuu, juhudi zetu, na nguvu zetu zielekezwe katika kusimamisha utawala wa Uislamu kupitia Dola ya Kiislamu, Khilafah, ambayo wakati wake umewadia na ambayo zama zake zimepambazuka, Mwenyezi Mungu akipenda. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu kulitimiza. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ]
“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.” [Al-Qasas: 5].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Syria |
Address & Website Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria www.tahrir-syria.info |
E-Mail: media@tahrir-syria.info |