- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Kitengo cha Wanawake “Kampeni ya Kimataifa - Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”
Mgogoro wa kikatili nchini Sudan kati ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan vinavyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mtawala mkuu wa Sudan, na Vikosi vya kijeshi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), naibu wa zamani wa Burhan katika Baraza la Utawala, sasa umeingia mwaka wa tatu. Baadhi ya makadirio yanaweka idadi ya waliouawa kuwa 150,000, na ukatili wa kutisha uliofanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, mateso, na ubakaji mkubwa. Mauaji ya kikabila na kikatili pia yameripotiwa katika miji mbalimbali, vijiji na kambi za watu waliohama. Vita hivyo vimesababisha mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu, mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi, na janga kubwa zaidi la njaa ulimwenguni, huku nusu ya watu milioni 50 wakikabiliwa na njaa. Hata hivyo, mzozo huu umeelezewa kuwa "vita vilivyosahaulika" na "mgogoro uliofichwa na usioonekana" kwa sababu haujapata usikivu wa kimataifa na utangazaji wa vyombo vya habari vya kimataifa unaostahili. Kwa hiyo, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua kampeni ya kimataifa kuangazia maafa yanayozidi kuwa mabaya ya kibinadamu yanayowakabili Waislamu wa Sudan. Kampeni hii pia itashughulikia: siasa na ajenda zilizofichwa nyuma ya mzozo huu, dola za kikanda na kimataifa zinazofadhili vita na sababu zake, historia ya Sudan na mambo yaliyosababisha migogoro ya hivi karibuni na kufeli kiuchumi, kwa nini mfumo wa kidemokrasia umefeli kutatua matatizo mengi ya kisiasa, kiuchumi, kikabila na kijamii ya Sudan, na jinsi uongozi wa Kiislamu wa Dola ya Khilafah Rashida, unaweza kujenga mustakabali mzuri wa Sudan na nchi nyingine za Kiislamu zenye mafanikio.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal: 24]
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Jumatatu, 10 Safar Al-Khair 1447 H sawia na 04 Agosti 2025 M
- Fuatilia Kampeni kwa Lugha Nyenginezo -
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari ya Kitengo cha Wanawake
ambayo ilitangaza uzinduzi wa kampeni yake ya kimataifa yenye kichwa:
“Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”
Jumatatu, 10 Safar Al-Khair 1447 H sawia na 04 Agosti 2025 M
Video ya Ualishi wa Uzinduzi wa Kampeni ya Kimataifa
“Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti, na Udanganyifu”
Kipeperushi cha Kampeni
Kupakua Nakala ya PDF Bonyeza Hapa
- Alama Ishara za Kampeni -
#أزمة_السودان
#SudanCrisis
#SudanKrizi
#SoudanCrise
Fuatilia Kampeni ya Kimataifa katika Mitandao ya Kijamii
Facebook: QANITATHT1
https://www.facebook.com/QanitatHT1
X: @ALQANITAT
Instagram: @WOMEN_SHARIA
https://www.instagram.com/women_sharia?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==