Jumamosi, 28 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  25 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 34
M.  Jumatano, 17 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Yakutana na Sheikh Farouq Al-Haj Abdullah Al-Sheikh Dafa’ Allah
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumanne, tarehe 16/09/2025, ujumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, ukishirikiana na Bw. Abdullah Hussein, mratibu wa kamati hiyo, na Sheikh Abdul Qader Abdul Rahman, mwanachama wa Hizb, ulikutana na Sheikh Farouq Al-Haj Abdullah Abdullah Al-Sheikh Dafa’ Allah, Katibu wa Sekretarieti ya Utamaduni wa Da’wah ya Kabila la Al-Kalaklat.

Mkutano huo ulijadili mpango wa nchi za Magharibi kwa ujumla wake, hasa Amerika, katika kutafuta kuchana kile ambacho tayari kimeshachanwa na Sykes-Picot mpya kwa mipaka ya damu. Na huu hapa ni mpango wake nchini Sudan baada ya kuitenganisha Kusini yake: sasa inataka kuitenganisha Darfur. Kinachotakiwa kutoka kwa watu wote wa nchi hii ni kufanya kazi ya kutibua njama hii, hususan wanazuoni ambao ni wajibu wao kusema ukweli, kuwaelimisha watu juu ya njama hii, na kutilia mkazo ufaradhi wa kufanya kazi kwa ajili ya umoja wa nchi, bali kazi ya kuziunganisha ardhi za Waislamu kwa jumla kwa kutoa bay’ah kwa Khalifa wa Waislamu.

Sheikh Farouq Al-Haj Abdullah aliushukuru ujumbe kwa ziara hii akisema: Mwenyezi Mungu azibariki juhudi na mapambano ya Hizb ut Tahrir. Alimuombea rehema Sheikh Ali Saeed, msemaji rasmi wa zamani wa Hizb, na akathibitisha umuhimu wa mawasiliano na ushirikiano katika mambo ambayo yanarekebisha hali ya Ummah, na akawasilisha kwetu ruwaza ya Sekretarieti ya Da’wah na Utamaduni kwa ajili ya uchunguzi na majibu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu