Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 8 Rabi' II 1447 | Na: H 1447 / 013 |
M. Jumanne, 30 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uacheni Umma Ufanye Uamuzi Wake, Enyi Watawala Waoga!
(Imetafsiriwa)
Hatukushangazwa, wala Umma wa Kiislamu haukushangazwa na ukaribishaji wa watawala wasaliti wa Waislamu wa mpango wa rais wa Marekani Donald Trump wa kuipoteza Gaza, kwani wao wametuzoezesha sisi kuwa waoga, badala ya kula njama na wakoloni makafiri dhidi ya masuala yetu. Trump alikuwa amekutana na baadhi yao jijini New York kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mnamo Jumanne tarehe 23/9/2025, na wakamsifu na kutangaza kumtegemea yeye kumaliza vita dhidi ya Gaza. Mara tu Trump alipotangaza mpango wake wa ukoloni, waliharakisha kuukaribisha. Wasingewezaje kuukaribisha, wakati hakuna hata mmoja wao aliyesubutu kufanya vyenginevyo, kwa kuwa wamepoteza ari na ushujaa wa wanaume.
Enyi Waislamu: Mumejua, bila shaka yoyote, kwamba Trump ndiye muungaji mkono mkuu wa umbile la Kiyahudi katika jinai zake za kutisha mjini Gaza na Ukingo wa Magharibi. Analipatia kila kitu linachohitaji kwa upande wa silaha, pesa, na habari, na kulipatia vyombo vya habari na habari na hifadhi ya kisiasa katika majukwaa ya kimataifa. Mumesikia kauli zake nyingi katika kuangazia uhalifu wake, kauli yake kuhusu eneo lake, kauli zake kuhusu Gaza na azma yake ya kuanzisha miradi ya kiuchumi ndani yake, na kuendelea kwake na Makubaliano ya Abrahim aliyowalazimishia juu ya watawala wenu. Muliyasikia maneno yake alipokuwa akitangaza mpango wake wa kikoloni pamoja na mhalifu Netanyahu: “Israel itakuwa na uungaji mkono wangu kamili ili kumaliza kazi ya kuangamiza tishio la Hamas,” kana kwamba hakuwa amefanya hivyo kabla na angali anafanya hivyo! Mumejua haya yote, kwa hivyo je, mhalifu kama huyo anaweza kuaminiwa maswala yenu? Na je inaweza kutarajiwa kutoka kwake kuzingatia maslahi yenu?
Enyi Waislamu, na enyi majeshi katika ardhi za Kiislamu:
Nyinyi mnahitaji mtawala anayemuiga Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika misimamo na sera zake, na anafanya kama Maswahaba watukufu, Mwenyezi Mungu awawie radhi, na wale waliowafuata kwa wema walivyofanya. Mtawala ambaye anasimama kama Abu Bakr, Umar, Harun al-Rashid, al-Mu‘tasim, Salah al-Din, Baibars, Qutuz, na Abdul Hamid. nyinyi mnahitaji mtawala ambaye, anaposema neno, husikika katika upeo wa macho wa dunia, na maadui hutetemeka kutoka humo—neno linalofuatwa na kitendo ambacho huwafanya maadui kusahau minong’ono ya Shetani. Ili Trump na wahalifu kama hao wasikufanyieni yale wanayofanya leo, bali wapige mahesabu elfu moja kwa ajili ya Khalifa wenu. nyinyi mnahitaji Khilafah ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliitolea bishara njema: Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inaifanyia kazi kuisimamisha. Basi njooni muifanyie kazi na kuiunga mkono, ili mupate heshima ya dunia na kufaulu Akhera. La sivyo, musipofanya hivyo, watawala wenu waoga watakupelekeni kwenye maangamivu na kukusalimisheni kwa maadui zenu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |