Jumanne, 07 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amiri wa Sasa wa Hizb ut Tahrir

Amiri wa Hizb ut Tahrir ni Alim, Sheikh Ata Abu Rashta (majina kamili ni Sheikh Abu Yasin Ata ibn Khalil ibn Ahmad ibn Abdul Qadir al-Khatib Abu Rashta). Ni mwanasheria, mwanachuoni na mwandishi wa Kiislamu.

Sheikh Ata Abu Rashta alizaliwa katika familia makini ya Kiislamu mnamo 1943 kijiji kidogo cha Ra’na katika eneo la Hebron ndani ya Palestina. Alishuhudia uharibifu wa kwanza wa Israel wa Ra’na mnamo 1948 na baada ya hapo kuhama na familia yake kwenda katika kambi ya wakimbizi iliyoko karibu na Hebron. Elimu yake ya msingi na ya upili alimalizia katika kambi ya wakimbizi. Kisha alipata shahada yake ya kwanza ya elimu ya upili mnamo 1960 kutoka katika shule ya Al Hussein Bin Ali mjini Hebron na baadaye kumaliza shahada yake jumla ya elimu ya upili katika shule ya Ibrahimiya jijini Jerusalem mnamo 1961. Sheikh Ata Abu Rashta kisha alijiunga na Kitengo cha Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri na kuhitimu na shahada ya uhandisi wa ujenzi mnamo 1966. Baada ya kuhitimu, Sheikh Ata Abu Rashta alifanya kazi katika biladi kadhaa za Kiarabu kama mhandisi mjenzi na kuandika kitabu kuhusu hesabu za idadi kuhusiana na ujenzi wa majengo na barabara.

Sheikh Ata Abu Rashta alijiunga na Hizb ut Tahrir katikati mwa miaka ya 1950 na moja kwa moja akaanza kutekeleza harakati za chama katika ulimwengu wote wa Kiarabu. Alifanya kazi kwa karibu na Sheikh Taqiuddin an-Nabhani, muasisi wa Hizb ut Tahrir na Sheikh Abdul Qadeem Zallum aliyekuwa amiri wa Hizb ut Tahrir kufuatia kifo cha Sheikh Nabhani mnamo 1977. Mnamo miaka ya 1980 alikuwa mwanachama mstari wa mbele wa Hizb ut Tahrir nchini Jordan na kuteuliwa kama msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir. Sheikh Ata Abu Rashta alicheza dori kubwa nchini Jordan wakati wa Vita vya Ghuba la Fursi alipoitisha mikutano ya waandishi wa habari, mihadhara na midahalo katika sehemu za umma kote nchini. Alijadili kuhusu uvamizi wa Iraq nchini Kuwait katika Msikiti wa Jerusalem jijini Amman ambako alitoa muhadhara kwa anwani Uvamizi Mpya wa Kimsalaba Katika Bara Arabu na Ghuba. Mara kwa mara alitiwa nguvuni na vyombo vya dola vya Jordan. Mnamo 1994, katika mahojiano, Sheikh Ata Abu Rashta alisema, “Kusimamisha Khilafah kwa sasa ni matakwa jumla miongoni mwa Waislamu, wanaotamani hili: ulinganizi wa serikali ya Kiislamu (Khilafah) umeenea nchini Misri, Syria, Uturuki, Pakistan, Algeria na kadhalika. Kabla ya Hizb ut Tahrir kuanza kazi yake kadhia ya Khilafah ilikuwa haijulikani. Lakini, chama hiki kimefaulu katika kumakinisha uongozi wake wa kifikra, na sasa kila mmoja anaimani na fikra zake, na anazungumzia kukihusu: hili liko wazi kupitia vyombo vya habari ulimwenguni kote”. Abu Rashta alikuwa amiri wa kiulimwengu wa Hizb ut Tahrir mnamo 13 Aprili 2003 kufuatia kifo cha Sheikh Abdul Qadeem Zallum. Tangu kuchukua uongozi wa Hizb ut Tahrir, amezungumza katika makongamano kote ulimwenguni ikiwemo Indonesia, Pakistan na Yemen.

Ifuatayo ni orodha ya vitabu vya Kiislamu alivyoandika:

Wepesi katika elimu ya tafsiri – Surah al-Baqarah

Wepesi wa kufikia elimu ya Usul

Migogoro ya Kiuchumi – uhakika wake na suluhisho lake kwa mtazamo wa Kiislamu

Uvamizi Mpya wa Kimsalaba Katika Bara Arabu na Ghuba Sera ya maendeleo ya viwanda na kuunda dola ya kiviwanda kwa mtazamo wa Kiislamu

Chini ya usimamizi wake, vitabu vifuatavyo vimechapishwa na Hizb:

Miongoni Mwa Mambo Yanayokuza Nafsiyyah ya Kiislamu

Masuala ya Kisiasa – Ardhi za Kiislamu Zilizovamiwa

Nyongeza katika kitabu: Fahamu za Kiislamu

Msingi wa Sera ya Elimu ya Dola ya Khilafah

Nguzo za Dola ya Khilafah

Daima anamuomba Mwenyezi Mungu (swt) Amuwezeshe ujasiri ili aweze kutekeleza majukumu yake katika hali ambayo inamridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw); daima anamuomba Mwenyezi Mungu (swt) auwezeshe Umma kupata dola ya Khilafah kupitia mikono yake, Bwana wetu ni Mwenye kusikia yote na atamjibu dua zetu.

Hatua alizochukuwa wakati wa uongozi wake zinajumuisha kutoa mwito kwa Waislamu mnamo Rajab 1426 H sawa na Septemba 2, 2005 M zikihusiana na tukio chungu la kuvunjwa kwa Khilafah miaka 84 iliyopita. Mwito huu ulibuniwa Indonesia, na kisha ukafuatiwa na ufukweni mwa Bahari ya Pacific katika Mashariki pamoja na ufukweni mwa Bahari ya Atlantic katika Magharibi katika swala za Ijumaa. Mwito huu ukauwathiri Umma pakubwa. Kwa kuongezea, amekuwa mchangamfu katika kupaza sauti yake ya Ukweli kwa kuendelea katika makongamano, semina na mijumuiko mingi ya Hizb ut Tahrir. 

Miaka ya mwanzo ya uongozi wake ilikuwa imejaa khair na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Aendelee kuzidisha baraka Zake katika uongozi wake. Kuna ishara za wazi za kupatikana kwa Nussrah chini ya uongozi wake kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt). Tunamuangalia kwa matumaini na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atutangazie ushindi Wake wakati wa uongozi wake, Ameen.

Uchajimungu wa Amiri huyu ni mfano wa pekee. Anajituma katika kazi yake na yuko makini daima kutekeleza majukumu yake katika hali bora. Amethibitisha uwezo wake wakati alipokuwa anafanyakazi katika afisi nyingi ndani ya idara za Hizb na kufaulisha majukumu yake katika hali bora. Baadhi ya huduma zakutambuliwa ni zile zinazojumuisha alizofanya alipokuwa Mwakilishi, Mo'atamad na Msaidizi wa Ameer aliyetangulia. Hii ni sababu inayomfanya kutambua majukumu yake anayoyabeba kama Amiri na anayafahamu vyema. Anafuatilia amali zote kwa uchangamfu, hivyo basi, Shabab anamuhisi uwepo wake katika kila wanalofanya, kazi iwe ndogo au kubwa kiasi gani. Na hivi ndivyo anavyo patiliza uwezo wa Shabab.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 18 Aprili 2020 21:31

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu