Nani Anasherehekea Maadhimisho ya Isra na Mi’raj?
- Imepeperushwa katika Palestina
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tawala za ulimwengu wa Kiislamu zinatoa wito wa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka huu, licha ya kuwa wametambua uwepo wa umbile linaloinajisi ardhi iliyobarikiwa ya Isra na Mi’raj. Wamesimama kando, wakishuhudia mito ya damu ya Wapalestina ikitiririka, mabomu yaliyosababisha nyumba kuwa vifusi, na uharibifu ulioharibu vitongoji, mazao, na vizazi. Wametazama huku hofu ikiwashika wazee na vijana, huku njaa isiyo kifani ikiwasibu, na huku baridi ikigandisha miguu na nyoyo za watu.