Alhamisi, 12 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  8 Rabi' I 1360 Na: BN/S 1447 / 04
M.  Jumapili, 31 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miradi ya Wamarekani – Mayahudi ni Miradi ya Jinai na Uhaini, Iwe Inatekelezwa na PLO au Wengine
(Imetafsiriwa)

Chaneli 5 ya Kiebrania, kama ilivyoripotiwa na Al Jazeera, ilitangaza ripoti iliyosema kwamba Netanyahu anafanya mkutano kujadili kuchukua nafasi ya Mamlaka ya Palestina pamoja na viongozi wa kikabila huko Al-Khalil (Hebron). Taarifa ilitolewa baadaye na Gavana wa Al-Khalil (katika kujibu mashauri yanayoendelea ya serikali ya uvamizi kuhusu kuitenganisha Al-Khalil kutoka kwa jiografia ya kitaifa na kuikabidhi kwa utawala wa kikabila).

Kutokana na hayo, sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tunaeleza na kuthibitisha yafuatayo:

1- Uwepo wa Mamlaka ya Palestina (PA) ulikuja chini ya udhamini wa Marekani na kwa idhini ya umbile la Kiyahudi kama sehemu ya mradi wa kisiasa uliojengwa juu ya kuisalimisha Ardhi Iliyobarikiwa kwa umbile la Kiyahudi na kutekeleza mahitaji ya usalama kwa manufaa yake. Ilitekeleza dori hii ya usaliti kwa ukamilifu zaidi, na rais wake alijivunia kuhusu hilo kwenye mikutano ya Jumuiya ya Kiarabu na kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa. Ikiwa Amerika na Mayahudi watapata badali ya baadhi ya watu wa PA au kumaliza Mamlaka ya Oslo na uanzishwaji wa PA mpya chini ya jina lolote, itakuwa ni upanuzi wa mradi wake wa kufuta sababu ya Palestina, iwe kupitia PLO au kupitia chombo chengine wanachounda. Wakati Marekani na Wayahudi walipoamua kummaliza Yasser Arafat na idadi ya watu watiifu kwake, walimleta Mahmoud Abbas na kundi pamoja naye ambalo lilifanya kazi chini ya usimamizi na uangalizi wa Jenerali wa Marekani Dayton. Mamlaka hiyo haikuwa chochote ila ni mkono wa usalama wa umbile la Kiyahudi. Endapo umbile hilo litamaliza huduma zake, haitakuwa kwa sababu ya heshima iliyochukuliwa na Mamlaka hiyo, bali kwa sababu dori yake imekamilika na kile lilichotaka kutoka kwake kilipatikana na kisha hutupwa pale ambapo wasaliti hutupwa baada ya kumaliza misheni yao. Chombo kitakacholetwa na uvamizi huo kitakuwa cha aina sawa na Mamlaka hiyo na hakitakuwa chochote ila chombo cha usalama kwa Mayahudi.

2- Watu wa Palestina hawakuichagua PLO, bali ililazimishwa kwao, kusalimisha sehemu kubwa ya Palestina kwa Mayahudi. Kuionyesha kama mwakilishi pekee halali wa watu wa Palestina kunaimarisha tu dori yake ya uhaini, isiyokubalika kwa yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Jaribio lolote la Mamlaka ya Palestina (PA) kutaka kutambuliwa uhalali wake kutoka kwa watu wa Palestina ni jaribio la kuhamisha mzigo na dhambi zake kwa watu wa Palestina, ambao hawana hatia.

3- Upande wowote unaofanya kazi na uvamizi huo, bila kujali jina lake, ni sehemu ya uvamizi na moja ya zana zake. Lebo zenye kung'aa zenye jina lolote humfanya msaliti kuwa msaliti, na haiwakomboi wale wanaoshirikiana na uvamizi huo kutokana na unyanyapaa wa aibu na fedheha duniani na Akhera. Ushirikiano wowote, iwe na PLO na Mamlaka yake au na chombo chengine chochote kilichoanzishwa na uvamizi huo, ni dhambi inayowaangukia wale walioridhika na kuifuata (njia hii) mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), na sio kwa wale wanaoikataa na wakaepushwa nayo. Yeyote anayetangaza uungaji mkono wowote kwa PLO, PA, au chombo chochote kilichoanzishwa na uvamizi amejiweka katika safu ya wasaliti na hawawakilishi watu au ukoo wao, hata kama wanadai kufanya hivyo.

Kwa kumalizia: Tunawalingania watu wa Palestina kwa jumla, na watu wa Al-Khalil na familia zake hasa, kwa wito wa Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” [Al-Anfal: 27].

Tunawaonya dhidi ya kudanganywa na Mamlaka ya Palestina, kwa kutangaza misimamo ya kuiunga mkono, shirika, au chombo chengine chochote kilichoanzishwa na Marekani na Mayahudi. Kutojua hakutoi udhuru wa uhalifu, na kukubali kunamaanisha tu kuwafuata wasaliti katika uhaini wao.

Kadhia ya Palestina haiwakilishwi na shirika wala kumilikiwa na ukoo. Bali ni kadhia ya Ummah mzima. Watu wa Palestina hawana haki zaidi nayo kuliko Waislamu wengine wote. Vivyo hivyo na wajibu wao juu yake. Ni kadhia ya Dini na Aqidah (imani), na kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa. Haitatatuliwa na dola dhaifu iliyo makuchani mwa uvamizi. Bali itakombolewa kwa mikono ya waumini wa kweli wa Umma wa Muhammad (saw). Itarudi kuwa ua na mwenge wa Ash-Sham, na itakuwa kitovu cha makaazi ya Uislamu, kama katika bishara ya Mtume (saw).

[وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْفَتْحُ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ * قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنْفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنْظَرُونَ * فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانْتَظِرْ إِنَّهُمْ مُنْتَظِرُونَ]

“Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli? Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula. Basi wapuuze, nawe ngonja; hakika wao wanangoja.” [As-Sajdah: 28-30]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu