Ijumaa, 11 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Musibabaishwe na Mikutano, Fungueni Mipaka

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Ligi ya Nchi za Kiarabu uliofanyika jijini Doha, mji mkuu wa Qatar, Rais Erdoğan alisema: “Tunafahamu kuwa Israel haitasimama katika muda mfupi isipokuwa itakabiliwa na hisia kali na vikwazo. Tunafahamu kwamba tunazo mbinu za kuzuia hili.” (Agencies 15.09.2025)

Maoni:

Leo, iwe viongozi wa umma watakusanyika Istanbul, Riyadh, Cairo, au Doha, kamwe mandhari haibadiliki: matangazo, sentensi ndefu, shutma, taarifa zinazoonyesha udhaifu, matamshi yaliyo mbali na masuluhisho, mistari iliyojaa diplomasia. La kusikitisha, ingawa mikutano hii haina athari yoyote katika kukomesha mauaji, uharibifu na njaa mjini Gaza, kurudiwa kwa kauli zile zile zisizo na athari za viongozi waliolevywa na madaraka na nyadhifa si lolote bali ni mpango wa kuficha kutoweza kwao.

Kwa muda wa miaka miwili, Gaza imehukumiwa kwa uharibifu usiokoma, na kauli za viongozi ambazo haziendi mbali zaidi ya maneno ya hasira tu zinawapa ujasiri mkubwa zaidi makafiri wa Kiyahudi. Kama Rais Erdoğan mwenyewe alivyokiri, kwa kweli wanamiliki zaidi ya mbinu za kutosha kukomesha umbile hili la mauaji ya halaiki. Ilhali, ukosefu wa utashi wa kutumia mbinu hizi hudunisha rasilimali zao nyingi na nguvu kuwa za bure. Utashi unashikiliwa mateka na uoga. Huku ujasiri ukitolewa kafara kwa hesabu za viti, ukandamizaji unaendelea kuongezeka.

Mikutano hii inayoitwa mikutano ya kilele haileti heshima bali ni udhalilifu kwa ummah. Leo watawala wa Ummah wako katika mshiko wa maradhi ya wahn. Kupenda dunia na tamaa ya madaraka inawaweka mbali na Gaza. Hofu ya kifo inawageuza kutoka kwenye barabara ya Jerusalem na Gaza. Kama, katika makumi ya mikutano ya kilele iliyofanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, watawala wa ummah wangeamua mara moja tu kufungua mpaka ili kuung'oa moyo wa umbile la Kiyahudi, mauaji ya leo na mauaji ya halaiki yangekwisha kabla ya kuanza.

Kwa kuzingatia upana wa kijiografia na utofauti ulio nayo, kutojali kwa makafiri wa Kiyahudi – ambao ni nukta tu ndani yake – kungechochea heshima yenu. Nyinyi, viongozi 57 mnaoamrisha mamilioni ya wanajeshi, badala ya kuyashinda magenge machache ya ugaidi, mumebaki mumekwama kwenye viti vyenu na kuchagua udhalilifu. Licha ya mashini zenu kubwa za vita, silaha zilizoko mikononi mwa idadi ndogo ya mujahidina zimekuwa na athari zaidi kwa umbile la mauaji ya halaiki kuliko nyinyi. Aibu ya hili haionekani kukusumbueni. Mwenyezi Mungu amezijaalia ardhi zetu rasilimali zisizohesabika juu na chini ya ardhi, lakini munajizuia kuzipeleka Gaza, iliyohukumiwa kifo kwa njaa, zisiwe pumzi ya uhai kwao. Wakati makafiri kwa hakika wameunda mpaka pamoja na makafiri wa Kiyahudi, nyinyi kwa upumbavu munatarajia masuluhisho kutoka kwa watekelezaji wa mauaji haya.

Waislamu wanaomiminika mabarabarani kwa ajili ya Gaza wanahisi uchungu wa kaka na dada zao, nao wanahuzunika. Lakini viongozi bado hawawezi kuchukua hatua bila ruhusa kutoka kwa nchi za Magharibi. Wakati damu ya Waislamu inamwagika, meli za biashara zatia nanga kwenye bandari ya ‘Tel Aviv’. Wakati watoto wanachanwa vipande vipande kwa mabomu, mahusiano ya kidiplomasia yanaendelea. Wakati jeshi la mauaji ya halaiki linajaribu kumeza Gaza yote, ukali wa maneno yenu unafichua tu usaliti wenu. Ikiwa kweli muna uwezo wa kumzuia kafiri wa Kiyahudi, basi nyinyi pia muna uwezo wa kuwazuia sio wao tu bali makafiri wote, hasa Marekani. Katika hali hiyo, kila sekunde mutakayopoteza itakukabilini na matokeo ambayo hamtaweza kuyahesabu.

Mwenyezi Mungu aujaalie umma wa Kiislamu viongozi ambao maneno na matendo yao yatakuwa moja, wanaojua uzito wa maneno yao na hawatasita kuyakusanya majeshi kwa tone moja tu la damu ya ummah, ambao wataweka heshima na utu juu ya kila kitu, ambao hawatatoa nafasi kwa wafanyibiashara wa diplomasia ya uwongo, ambao watajibu mara moja na ipasavyo kwa makafiri waharibifu na ambao watakuwa waaminifu na chanzo cha usalama kwa umma.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu