Ijumaa, 11 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  8 Rabi' II 1447 Na: BN/S 1447 / 05
M.  Jumanne, 30 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mpango wa Trump ni Sumu Hatari, Ukaliaji Kimabavu wa Marekani na Umoja wa Mataifa wa Gaza, na Uhalifu Mkubwa Uliofanywa na Watawala wa Waislamu
(Imetafsiriwa)

Kujisalimisha na kutoa silaha, kuregeshwa kwa mateka na mabaki ya wafu, na uvamizi unaoongozwa na Marekani, inayoongozwa na Trump kwa jina la Baraza la Amani, likisaidiwa na mwenye chuki dhidi ya Uislamu, Tony Blair, na kutekelezwa na tawala za eneo hili – hizi ndizo sifa za mpango mpya wa Trump, ambao aliutangaza. Amewashukuru viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na washirika wake barani Ulaya kwa mwitikio wao wa dhati kwake, na kutangaza kuwa viongozi wa eneo hilo wanashiriki kikamilifu katika mpango huo wa amani.

Gaza, iliyolifedhehesha umbile la Kiyahudi na kufichua kwamba ni umbile dhaifu ambalo linahitaji uamuzi mmoja tu wa kuliondoa. Ili umbile hilo la kihalifu lirudishe fahari yake, lilimwaga nguvu zake zote kwa watu wa Gaza. Amerika na Magharibi zililipatia kila silaha ya kuua. Watawala wa Waislamu walilisaidia kwa kila walichoweza, kuanzia njia za usambazaji mahitaji na mzingiro, na njia nyenginezo, ili liregeshe tena ile fahari inayodaiwa. Gaza iliharibiwa kabisa, au karibu iangamizwe, na watu wake walizingirwa kwa mzingiro usio na kifani. Licha ya hayo, umbile halifu lilishindwa kufikia ushindi wake uliotaka katika eneo lililozingirwa ambapo kulikuwa na mabaki ya uhai. Kisha kamba ya Trump ikaja kuwaokoa Mayahudi, wakisaidiwa na watawala wa Waislamu, kwa mpango wa kukaza mshiko wao huko Gaza, wakiwataka Mujahidina waukubali. Haya yote ni ili Trump aweze kufanikisha kwa umbile hilo ovu kile ambacho halijafanikiwa kwa miaka miwili, na kuzifanya tawala za madhara katika nchi zetu kuwa chombo cha utekelezaji, baada ya kuibwaga Gaza na watu wake kwa miaka miwili kamili. Matokeo yake yalikuwa ni kuisalimisha Gaza kwa Trump bila juhudi yoyote, na hata kwa pesa na wanajeshi wa Ummah!

Trump anapanga kwa ajili ya Gaza kana kwamba ni yake, na watawala vibaraka wanafurahi kuisalimisha kwake, kana kwamba wamesaidia watu wake. Wamesuka nyuzi za kujisalimisha kwake pamoja na bwana wao, na kuigeuza kuwa mradi wa uvamizi wa kimataifa – uvamizi kwa jina la ujenzi upya juu ya mito ya damu na milima ya mafuvu na mifupa!!

Kisha, kuisalimishwa Gaza kutakuwa utangulizi wa uhalalishaji mahusiano na Mkataba wa Abraham, kuruhusu umbile halifu kupenya katika eneo hili, kana kwamba linalipwa ujira kwa uhalifu wake.

Kukubali mpango wa Trump ni uhalifu ambao mzigo wake uko kwa watawala. Lakini pia ni mzigo ambao Ummah wa Kiislamu hautasalimika isipokuwa ubadilishe njia zake na kukemea jinai zao.

Zaidi ya hayo, ni mzigo ambao majeshi ya Ummah, ambayo yamechelewa kutekeleza wajibu wao, hayatasazwa. Lau majeshi hayo yangetiwa moyo na ushujaa wa Gaza na kufidia kuchelewa kwao kuikomboa Al-Quds na viunga vyake, na lau yangeitikia wito wa msaada kutoka Gaza na viunga vyake, Trump asingepata nafasi kwa ajili ya mpango wake huo, wala hangeota chembe ya mchanga katika Ukanda wa Gaza wa Hashem.

Hata hivyo, fursa hiyo bado haijapita, hata ikiwa imechelewa, kwani Gaza, pamoja na wanaume na wanawake wake, wazee na vijana wake, misikiti na minara yake, inalilia majeshi yasonge, kuikomboa Al-Quds kwa harakati zake, ili kuzuia watawala wasihalalishe mahusiano juu ya mafuvu na mifupa ya Gaza, kuregesha Msikiti wa Al-Aqsa na ardhi iliyobarikiwa kama ilivyokuwa moyo, yenye heshima na isiyopenyeka, na hata kuifanya Al-Qudsi moyo wa nyumba ya Uislamu.

Tunamalizia kwa wito wa Mwenyezi Mungu kwa Waumini:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ * فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَنْ تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَنْ يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِنْ عِنْدِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu * Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma’idah: 51-52].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu