Suluhisho la Dola Mbili ni Kejeli ya Karne isiyo na Aibu
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inashutumu vikali kile Prof. Yunus alisema kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, “Ni kwa msingi wa mipaka ya kabla ya 1967 tu, na Israel na Palestina wakiishi bega kwa bega kwa amani, haki inaweza kutendeka”. Wakati watu wa Palestina wanaangamizwa mbele ya macho yetu na Mayahudi kunyakua 78% ya Palestina kinyume cha sheria, ni vipi haki inaweza kutendeka kwa kuruhusu ‘Israel’ kuishi bega kwa bega na Palestina! Kwa nini tunaita makundi machache ndani ya umbile haramu la Kiyahudi kuwa ni dola (Palestina), lakini haina hata jeshi lake?