Jumatatu, 17 Safar 1447 | 2025/08/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  12 Safar 1447 Na: H 1447 / 07
M.  Jumatano, 06 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tarehe 5 Agosti 2024 ni Siku ya Uasi wa Watu dhidi ya Dhalimu na Utawala wa Kidhalimu, ambao ungali Unaendelea; kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni Hati ya Usaliti wa Vyama vya Kisiasa vinavyounga mkono Marekani ili kuangamiza Uasi wa Watu

(Imetafsiriwa)

Wananchi wakiwa wamekata tamaa sana, wamepita mwaka mmoja tangu kuanguka kwa Hasina katika uasi mkubwa dhidi ya dhalimu Hasina na utawala dhalimu mnamo Agosti 5, 2025. Kwa sababu baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, vibaraka wa Marekani na vyama vya kisiasa vyenye uchu wa madaraka vimechukua mshiko wa kubainisha hatima ya watu na kuweka vikwazo katika kutekeleza matumaini na matarajio ya watu na wameendelea na majaribio yao maovu na kuteka nyara uasi huo. Kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni hatua isiyo na aibu ya jaribio hili ovu. Watu wamekataa utumwa wa Marekani na sarakasi za kisiasa kwa chuki. Yaliyo mbali na kuakisi matarajio ya watu, Tangazo hili la Julai halitambui hata matukio kama vile njama ya India huko Pilkhana na mauaji ya halaiki ya watu wanaopenda Uislamu huko Shapla Chattar. Sabiini na moja (71), sabiini na tano (75), tisiini (90) ni maregeo yao, ambayo kwayo uso wa tabaka tawala umebadilika; lakini hatima ya watu haijabadilika, kwa sababu mfumo mzima wa utawala haujabadilika. Kwa hakika, umetungwa ili kuhifadhi mwendelezo wa mfumo wa sasa wa kibepari wa kisekula, na kukubali utawala wa Marekani na wapambe wake wa kikanda India. Wananchi pia walilazimika kushuhudia kwamba uongozi wa wasaliti wa vuguvugu la kupinga ubaguzi, ambao walidai kuwa kiongozi wa vuguvugu la wanafunzi, walikuwa Cox's Bazar siku ya Tangazo la Julai, wakifanya karamu ya kusherehekea pamoja na Peter Haas.

[قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ]

“Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surah Munafiqun: 4].

Tunapenda kuwakumbusha wasomi na wanasiasa wanaougua homa ya demokrasia kwamba demokrasia yenyewe ni udikteta, kwa sababu inawapa watu mamlaka ya kujitawala. Lazima mujue kuwa Abraham Lincoln, anayechukuliwa kuwa rais mkuu zaidi wa kidemokrasia duniani, alisitisha sheria za kiraia katika baadhi ya maeneo mnamo 1861 na kuibuka kuwa dikteta kwa kukiuka Katiba. Mnamo 1862, alisitisha sheria ya habeas corpus na kuwafunga 'Wanademokrasia wa Copperhead' elfu kumi na tatu chini ya sheria ya kijeshi kwa sababu walipinga vita. Wakati Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo alipotangaza vitendo hivi vya Lincoln kuwa kinyume na katiba, Lincoln alitoa hati ya kukamatwa kwa Jaji Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 84. Ni wazi kutokana na tukio hili kwamba hata mizani ya utawala irekebishwe kiasi gani kwa kuleta mageuzi katika mfumo wa sasa, watawala wanaotawala wanabaki katikati ya madaraka; na mabwana zao wakoloni, Wamarekani, watawaunga mkono maadamu wanaweza kuwakalia watu. Iwapo wananchi watawaangusha watawala wakuu kupitia uasi, Wamarekani watateka nyara tena vuguvugu la watu kwa kutoa ahadi tupu za demokrasia. Uhalisia huu umeshuhudiwa na watu wa nchi hii kwa miongo kadhaa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلَالاً بَعِيداً]

“Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali” [Surah An-Nisa: 60].

Watu wa nchi hii pia wameshuhudia utawala wa kidemokrasia, hivyo moja ya matakwa ya wananchi baada ya mapinduzi ya wananchi ni kuitupilia mbali katiba ya kisekula na kuanzishwa katiba ya Kiislamu. Serikali ya mpito, vikiwemo vyama vya kisiasa vilivyo tiifu kwa Marekani, vimeweka wazi msimamo dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kuyataja matakwa ya kuanzishwa Khilafah tukufu kuwa yenye misimamo mikali na kutoa dhamira yao ya kukabiliana na misimamo mikali kwa Marekani. Mbali na kuimarisha jeshi la nchi hiyo kukabiliana na nchi adui India, badala yake wamezaa mkasa wa Pilkhana. Kwa hakika, India ni mojawapo ya washirika wa Marekani katika eneo la Indo-Pacifiki, hivyo vyama vya kisiasa vinavyounga mkono Marekani vinatabanni sera yao ya kupiga magoti kuelekea India. Watu wa nchi hii wameipa mgongo demokrasia na vyama hivi vya khiyana vya kisiasa, na kuungana katika mapambano ya kusimamisha mfumo wa Kiislamu yaani Khilafah. Mfumo ujao wa Khilafah pekee ndio utakaoweka katiba ya Kiislamu, kuhakikisha haki adilifu za watu, na kuikomboa nchi kutokana na utawala wa mkoloni kafiri Marekani, na kuichukulia India kuwa Dola adui na kung'oa ushawishi (mguu) wote wa India kutoka katika nchi hii.

[... فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنْ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلاَ يَضِلُّ وَلاَ يَشْقَى]

“…Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” [Surah Ta-Ha: 123].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu