Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wanaozuru Ukurasa wake kwa Mnasaba wa Idd ul Fitr iliyobarikiwa ya Mwaka 1446 H sawia na 2025 M
- Imepeperushwa katika Hotuba
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ndugu na Dada Wapendwa: Idd hii inakuja na dola ovu ya Kiyahudi inafanya ukatili dhidi ya watu, miti na mawe huko Gaza na Palestina yote, inafanya hivyo kwa msaada wa Marekani, ambayo inaipatia mabomu, makombora na ndege. Ingawa si ajabu kwamba umbile la Kiyahudi kwa kuungwa mkono na Marekani linatekeleza hili, kwani wao ni adui wa Uislamu na Waislamu, lakini cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja wa watawala katika nchi za Kiislamu anayechukua hatua, hasa wale walioko pambizoni mwa Palestina, ili kuyakusanya majeshi yao kuinusuru Gaza, watu wake, Al-Aqsa, na viunga vyake, na kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, na kisha kuiregesha Palestina yote kwa watu wake. Je, yule anayeikalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu na akawatoa watu wake humo hastahiki kupigwa vita na majeshi ya Waislamu na kufukuzwa humo kama walivyowafukuza watu wake?