Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
Date  :   1 Shawwal 1445   -    Jumatano, 10 Aprili 2024 No: 02/1445

Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wanaozuru Ukurasa wake kwa Mnasaba wa Idd ul Fitr iliyobarikiwa ya Mwaka 1445 H sawia na 2024 M
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na maswahaba zake, na wanaomfuata.

Kwa Umma wa Kiislamu, umma bora zaidi kuwahi kuletwa kwa wanadamu:

[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aal-i-Imran: 110].

Kwa wabebaji wa Dawah walio safi na wachamungu, “Na hatumsifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu,” wanaosema maneno mema na kufanya vitendo vyema. Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu wale wenye sifa hizi.

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين...]

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?” [Fussilat: 33].

Kwa watukufu wanaozuru ukurasa wanaoukaribia kwa ukweli na ikhlasi, na wanaotafuta wema unaowaletea, Mwenyezi Mungu awalipe mema.

Nawapongeza nyote kwa sikukuu njema ya Idd Al-Fitr... na Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie amali zenu njema.

Hakika Mwenyezi Mungu (swt) huwachunga watu wema.

Ndugu na Dada Wapendwa:

Idd hii inakuja na dola ovu ya Kiyahudi inafanya ukatili dhidi ya watu, miti na mawe huko Gaza na Palestina yote, inafanya hivyo kwa msaada wa Marekani, ambayo inaipatia mabomu, makombora na ndege. Ingawa si ajabu kwamba umbile la Kiyahudi kwa kuungwa mkono na Marekani linatekeleza hili, kwani wao ni adui wa Uislamu na Waislamu, lakini cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja wa watawala katika nchi za Kiislamu anayechukua hatua, hasa wale walioko pambizoni mwa Palestina, ili kuyakusanya majeshi yao kuinusuru Gaza, watu wake, Al-Aqsa, na viunga vyake, na kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, na kisha kuiregesha Palestina yote kwa watu wake. Je, yule anayeikalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu na akawatoa watu wake humo hastahiki kupigwa vita na majeshi ya Waislamu na kufukuzwa humo kama walivyowafukuza watu wake?

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni,” [Al-Baqara: 191]. Je, watawala hawatambui hili?! Bali masaibu yao yamewatawala, kwani utiifu wao ni kwa wakoloni makafiri, haswa Marekani, hawakatai amri zake zozote ili kuhifadhi viti vyao vibovu vya utawala. [قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُون] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun: 4]

Ndugu za Dada:

Vita hivi vinafichua mambo mawili muhimu:

La kwanza ni udhaifu na udhalilifu wa Mayahudi, kama alivyowataja Mwenyezi Mungu (swt) katika Kitabu Chake:

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ]

“Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu.” [Aal-i-Imran:112]. Walikata kamba ya Mwenyezi Mungu baada ya Mitume wao, na hakuna kilichobakia kwao isipokuwa kamba ya watu, Marekani na wafuasi wake. Watu wa aina hii si watu wanaostahili ushindi katika vita. Zaidi ya miezi sita imepita tangu uvamizi wao wa kikatili dhidi ya watu wa Gaza, bila ya kufikia malengo yao, ingawa wanapigana na kundi ambalo ni ndogo zaidi kwa idadi na vifaa.

Pili ni usaliti wa watawala katika nchi za Kiislamu.

Wanatazama kinachoendelea. Mbora miongoni mwao ni yule anayehesabu idadi ya mashahidi na majeruhi. Hawakukusanya majeshi kuinusuru Gaza na watu wake, kana kwamba jambo hilo haliwahusu! Au hawana upande wowote, au karibu na adui.

[صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ] “Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.” [Al-Baqara: 18].

Mambo haya mawili yanapaswa kuwasukuma wenye ikhlasi na watu wenye nguvu katika majeshi ya Kiislamu kutangaza mkusanyiko jumla ili kutimiza wajibu wa Mwenyezi Mungu wa kupigana na Mayahudi wanaoikalia kwa mabavu Palestina.

[وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ إِنْ تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ وَتَرْجُونَ مِنَ اللهِ مَا لَا يَرْجُونَ]

“Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao.” [An-Nisa: 104]. Hivyo basi muliondoe umbile lao, kwani wao ni duni zaidi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuliko kushinda katika vita, na ndipo itatimia ahadi ya Mwenyezi Mungu.

[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

“Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra: 7].

Basi, kimbiliani kuwanusuru ndugu zenu wa Gaza, na ikiwa tawala za kidhalimu katika nchi za Kiislamu zitasimama dhidi yenu, basi waondoeni kwa njia zote... na msimamishe utawala wa Mwenyezi Mungu badala yao, Khilafah kwa njia ya Utume, katika kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ»

“Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu (ملكًا جبرية) utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.’ Kisha akanyamaza (saw).” [Musnad ya Imam Ahmad]. Kisha Khalifa, wasaidizi wake, na askari wa Uislamu, kutoka daraja la juu hadi la chini kabisa, watatoka kwenye ushindi hadi kwenye ushindi, huku wakipiga takbira “Allahu Akbar” na Ummah kupiga takbira “Allahu Akbar” pamoja nao, kwa nguvu na msaada wa Mola wao Mlezi na kujivuna kwa Dini yao, hivyo hakuna adui atakayesubutu kusimamisha umbile katika ardhi ya Uislamu.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Kwa kumalizia, ndugu zangu na dada zangu, nawapongeza sana kwa sikukuu ya Idd al-Fitr, nikimuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie kwamba tumetekeleza swala na saumu na qiyam ya mwezi huu mtukufu kwa njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) . Pia namuomba (swt) kwamba Idd hii iwe mwanzo wa kheri, baraka na utukufu kwa Uislamu na Waislamu.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُون]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21].

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ndugu Yenu
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

1 Shawwal 1445 H

Sawia na 10/4/2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu