Msamaha Mbele ya Mola Wetu, na Pole kwa Waliojeruhiwa Gaza Tripoli ash-Sham Yapaza Sauti Yake Dhidi ya Sherehe za Kucheza juu ya Majeraha ya Umma!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon imetoa wito kwa Mashababu (wanachama) wake kushiriki katika kikao kilichopangwa kwa uratibu na wanaharakati na watu mashuhuri katika mji wa Tripoli, Jumamosi hii jioni saa sita kamili mbele ya Maonyesho ya Kimataifa ya Tripoli, kwa ajili ya kukemea tamasha la densi (Zambo) na kuimba katika mji wa Tripoli, mji wa elimu na wanazuoni, kama udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusiana na makosa yanayofanywa mjini Tripoli na ambayo hayaonyeshi kitambulisho chake, katika wakati ambapo umbile halifu la Kiyahudi linaendesha vita vikali dhidi ya Waislamu wa Palestina kwa jumla na hasa Gaza, na uvamizi na jinai zake zimeenea hadi Lebanon na Syria, kwa kukalia kimabavu sehemu ya ardhi ya Kusini na ardhi ya Syria, na ndege zake hazijaondoka anga zake, zikipiga mabomu na kuangamiza bila kuzuiwa au mwenye kuwazuia!